Kufuatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuutangazia umma kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liliokuwa lianze tarehe 04/07/2015 kwa Jiji la Dar es Salaam na tarehe 25/06/2015 kwa mkoa wa Pwani kwamba limeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa tena; Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda Pwani (Mikoa ya Temeke, Kinondoni, Ilala na Pwani) kinaitaka Tume ifanye yafuatayo:
1.Tume ya Uchaguzi itangaze tarehe ya kuanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani baada ya kuahirishwa ili kuwasaidia wananchi kujipanga kwa zoezi zima la uandikishaji.
2.Tume ya Taifa ya Uchaguzi izingatie mfumo wa kiuchumi na kimazingira uliopo katika
mikoa hii unaowafanya watu wengi muda
wa mchana kuwepo makazini/katika shughuli za
kiuchumi. Na kupanga muda wakutosha kwa kuzingatia
idadi ya wakazi. Hii ni pamoja na
kuzingatia kuwa Jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani pekee, kwa takwimu za serikali, vina wapiga kura wapatao asilimia 15 ya wapiga kura wote nchini.
3.Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ihakikishe
changamoto zote zilizotokea sehemu mbalimbali zinapatiwe ufumbuzi kabla ya zoezi halijaanza Dar es Salaam na Pwani. Changamoto hizi ni pamoja na; mashine kuwa mbovu, idadi ya mashine kutokukidhi
mahitaji, idadi ya vituo kwenye kata
kutoendana na idadi ya wanaotakiwa
kujiandikisha, utaratibu wa kuchukua majina
bila kuzingatia waliopanga mistari, na waandikishaji kutokuwa na uwezo thabiti wa kutumia mashine
za uandikishaji. Uzoefu umeonyesha kuwa,
changamoto hizi zimeendelea kujirudiarudia katika sehemu nyingi bila kutolewa ufumbuzi wa uhakika na Tume ya Uchaguzi.
4.
Tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka wazi mbele ya umma kuwa Jeshila
Polisi halihusiki katika kupanga utaratibu wa BVR hali inayosababishavurugu na ukosefu wa amani vituoni. Uzoefu uliopatikana wakati wa ziara za viongozi wakuu wa chama kukagua zoezi la BVR katika maeneo mbalimbali unaonesha kuwa maeneo yote ambayo polisi hawakuwepo vituoni wakati wa uandikishaji,
utaratibu ulikwenda kwa utulivu lakini hali
imekuwa tofauti kabisa kote ambako jeshi hilo limehusika kusimamia uandikishaji
Mf; Arusha Tunapeda
kusisitiza kuwa; CHADEMA haitofumbia macho
mikakati yoyote itakayoonekana ina dhamira
ya kudhoofisha zoezi la uandikishaji ambayo itasababisha
kuwanyima wananchi haki ya kikatiba ya
kupiga kura, maana bila kujiandikisha mtu hawezi kupiga kura.
Mwisho,
CHADEMA inapenda kuwahamasishwa wananchi
kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la uandikishaji litakapoanza katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Asanteni!
IMETOLEWA NA Mhe. MABAERE N. MARANDO MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA PW
No comments:
Post a Comment