.

SENTENS TISA NILIZONUKUU KUTOKA KWA LIPUMBA LEO

PICHA NA MAKTABA.
Story kubwa leo katika Jiji la Dar es salaam hususani katika tasnia ya siasa ilikuwa ni mkutano mkubwa uliofanyika katika ukumbi wa ubungo plaza wa chama cha wananchi CUF mkutano uliokuwa na lengo la kumkabidhi form ya kuomba ridhaa ya kugombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho ambapo mgombea alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho mwenyewe Profesa IBRAHIM HAROUNA LIPUMBA.
Hapa nimekuwekea baadhi ya sentens ambazo mwenyekiti huyo alizizungumza katika hotuba yake ya kuomba ridhaa ya wanachama wa chama hicho ili jina lake liweze kupelekwa katika meza ya UKAWA.

1-Watu wanauliza kwanini nangangania kuchukua form kwa mara ya tano tena,mwaka huu ni tofauti sana na chaguzi ziingine,ni mwaka wa kufanya maamuzi ya ukweli juu ya nchi yetu,nachukua form kipindi ambacho nchi ipo katika hali mbaya ya kiuchumi na iko wazi kuwa sasa nchi imechoka.

2-Mimi ni mchumi ambaye nimetumika sana na mataifa m
akubwa katika kuwashauri katika maswala ya kiuchumi na wakafanikiwa kupitia kwangu,nadhani sasa ni wakati wa kujenga uchumi wa Tanzania yangu mimi nikifanikiwa kuwa Rais ntahakikisha tunajenga uchumi utakaomsaidia kila mtanzania.

3-Ntahakikisha kuwa watoto wa Tanzania wanapata fursa ya kupata matunzo ya uhakika,ntasimamia katika lishe ya watoto na mama wajawazito ili tujenge taifa imara,tofauti na sasa ambapo watoto wa Tanzania muonekano wa vimo vyao haulingani hata kidogo na umri wao,wengi wanakosa lishe bora wakiwa wadogo na hakina anayeliona hilo kwa sasa.

4-Suala la ajira ni tatizo kubwa sasa,nkifanikiwa kuiongoza Tanzania ntahakikisha kuwa tunatengeza mazingira yatakayotoa fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania kwa wingi.tutahakikisha swala la miundombinu linarejkebishwa kwani ndio msingi wa kutengeneza ajira,kama tukiwa na miundombinu bora najua maswala ya gesi na kilimo vitafika kila eneo na ajira zitakuwepo kwa wingi.

5-Hali ya afya Tanzania ni mbaya sana,bado kuna matatizo makubwa sana katika secta ya afya,Tanzania inahitaji hifadhi ya jamii hususani kwa wazee wa Tanzania bado wanateseka sana na swala la afya.

6-Maswala ya ufisadi nchini Tanzania ni Tatizo sugu ambalo serikali ya ccm wameshindwa kulifanyia kazi,hao wanaotuibia kila siku ndio hao wako mtaani wanatangaza nia,wangetakiwa wote wawe jela wanatumikia kifungo.mimi nikichukua hii nchi sitacheka na mafisadi kama hao nakamata wote naweka ndani.
7-Swala la katiba mpya ntahakikisha tunauanza mchakato upya huku tukiyaheshimu maoni yaliyotolewa na wananchi na sio matakwa ya watu flani.

8-Kama UKAWA wakimchagua mtu mwingine kusimama katika nafasi ya urais naahidi kuwa ntakuwa naye bega kwa bega kumpigania hadi tuikomboe Tanzania.

9-Mwisho namaliza kwa kusema kuwa watanzania tuende tukajiandikishe kwa wingi katika daftari la kudumu la wapiga kura ili mwaka huu uwe ni mwaka wa maamuzi kweli.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.