Sunday, June 28, 2015

WAISLAM WAONYESHA KUCHOSHWA NA HALI YA TAIFA LA PALESTINA,SOMA WALICHOKISEMA LEO

Kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA akizungumza wakati wa semina hiyo
Waumini wa dini pamoja na viongozi mbalmbali na viongozi wa kitaifa katikia nchi zote duniani wametakiwa kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na kutengwa na mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA  wakati wa semina ya maimam na mashekh kuhusu QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi wa taifa la palestina na mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo yamekumbwa na machafuko makubwa kipindi cha karibuni.
Baadhi ya picha za matukio mbalimbali kutoka katimka machafuko huko Palestina
Akizungumza kwa uchungu kiongozi huyo amesema kuwa mataifa mbalimbali pamoja na mashirika makubwa ya kutoa misaada kama umoja wa mataifa yamekuwa hayana msaada wowote kwa taifa la palestina jambo ambalo limeendelea kuwaumiza watu wa taifa hilo na kuendelea kukandamizwa na mataifa ya Israel na mataifa mengine yanayowazunguka.
Amesema kuwa Taifa la palestina ni Taifa ambalo lina mchanganyiko wa dini na madhehebu mbalimbali hivyo wanaoumia katika dhuluma hizo ni watu wa dini zote huku akitanabaisha kuwa kuna haja ya wakristo na waislam nchini na duniani kuungana kwa pamoja kupinga kwa kasi kubwa dhuluma hizo wanazofanyiwa Taifa la palestina.
Viongozi mbalimbali wa Dini ya kiislam waliohudhuria semina hiyo
Amesema kuwa Palestina ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa duniani,na ni alama ya dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku akisema kuwa ndani ya taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa wapelestina ni dhuluma kwa dini zote wakristo pamoja na waislam.
Amesema kuwa kwa sasa wajibu mkubwa wa viongozi wa kidini na wapinga dhuluma kote nchini ni kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea katika mataifa hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla.
Nje ya semina hiyo
Semina hiyo ambayo imewakutanisha maimam pamoja mashekh mbalimbali imefanyika Jijini Dar es salaam kwa kuandaliwa na (Tanzania ithnasheriya TIC pamoja na hawzar imam swadiq yani chuo cha imam swadiq kilichopo kigogo post jijini Dar es salaam.
Akizumgumzia malengo ya kufanyika kwa semina hiyo  kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania shekh HEMED JALALA amesema kuwa ni kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa wajue kuwa na taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo lakini wanaikosa hivyo watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia.

No comments: