WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA
MAALUM DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MMILIKI WA SHULE YA MTAKATIFU ZION
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma
za mauaji ya mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion iliyopo maeneo ya Ununio, Mbezi Beach wilaya ya
kipolisi Kawe mkoa wa kipolisi wa Kinondoni aliyejulikana kwa jina la ANNA D/O
MIZINGI, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Boko.
Mnamo tarehe
02/02/2015 majira ya saa za mchana mtoa taarifa alifika kituo cha Polisi na
kueleza kwamba marehemu ANNA D/O MIZINGI aliondoka tangu tarehe 26/12/2014
majira ya saa 1:00hrs akiwa na mmoja wa watuhumiwa wakitumia gari dogo aina ya
Toyota Verosa ambayo namba zake hazikufahamika mara moja iliyokuwa inamilikiwa
na marehemu na tangu wakati huo hakuwa ameonekana tena.
Kutokana na taarifa
hizo Jeshi la Polisi lilifungua jalada la uchunguzi na kuanza uchunguzi mara
moja. Wakati uchunguzi ukiendelea zilipatikana taarifa zilizosaidia kukamatwa
kwa watuhumiwa hao huko Uchira Miwaleni, Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Watuhumiwa walipokamatwa
na kuhojiwa mtuhumiwa mmoja kati ya hao watatu amekiri na kutoa maelezo kuwa
siku ya tukio aliondoka na marehemu kuelekea katika shule ya Mt. Zion. Kwamba walipofika
shuleni hapo walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa lakini yeye
alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule hiyo. Amesema akiwa katika
uzio huo aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga marehemu ANNA D/O MIZINGI na kisha
kumtupa katika shimo la choo. Baada ya kitendo hicho watu waliotenda uhalifu huo
waliondoka na gari la marehemu na kutokomea kusikojulikana.
Tarehe 22/06/2015
mabaki ya mwili wa marehemu ANNA D/O MIZINGI yalipatikana eneo la Ununio baada ya
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Zima moto kubomoa shimo la choo
cha shule hiyo.
Watuhumiwa
waliokamatwa ni hawa wafuatao:
1.
DANIEL S/O RANADHANI MKILINDI @ ABDALLA
@ DULLA, Miaka 25, Mganga wa kienyeji, Mkazi wa Uchira Moshi – Kilimanjaro.
2.
SAID S/O RASHID OMARY @ SAID NTIMIZI au
DUVII, Miaka 34, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbweni JKT.
3.
ERICK S/O MZIRAY, Miaka 40,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Kurasini.
Watuhumiwa hawa
wanaendelea kuhojiwa ili kupata undani wa tukio hili ikiwa ni pamoja na
kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaohusiana na tukio hili.
Mara baada ya
uchunguzi kukamilika jalada la shauri hili litapelekwa kwa mwanasheria wa
serikali kwa hatua zake za kisheria.
No comments:
Post a Comment