Thursday, July 30, 2015

Habari Za Kimichezo Leo Nchini Tanzania



NUSU FAINALI KAGAME KIINGILIO BUKU TATU TU
Hatua ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Taifa, huku kiingilio cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni shilingi elfu tatu (3,000).

Viingilio vingine vya michezo hiyo ya kesho  ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa.


Timu nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya ijumaa.

Mchezo wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji nafasi ya kusonga mbele hatua ya fainali.

Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita, sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.

Kocha Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi dhidi ya Khartoum.

Kwesi Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu, Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin Ibrahim.

Vita kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman wote wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.

Nusu fainali ya pili itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi  ya Mamlaka ya jiji la Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na Kati katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na nahodha wake John Bocco.

KCCA chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.

Kocha Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na Muzamil Mutyaba.

Azam FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.

Hall atashuka dimbani akiwategema nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na mlinda mlango Aishi Manula.


TFF YAIPONGEZA AZAM FC
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salam.

Katika salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi pekee wa nchi kwenye michuano hiyo

TFF kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.

TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Moshi Shaban, kufutia kifo cha Moshi kilichotokea jana jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Moshi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa

Marehemu Moshi Shaban ni baba wa wachezaji waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Haruna Moshi “Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).


TFF YAANDAA KOZI YA WAAMUZI WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2015/2016

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa kozi ya waamuzi wa mpira
wa miguu watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza 2015/2016, kozi hiyo itafanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21 -24/08/2015.

Washiriki wa kozi hii ni waamuzi waliochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45 kwa wanawake na
miaka 23 – 45 kwa wanaume. 

Waamuzi wote wanatakiwa kuripoti tarehe 21/08/2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume Ilala Dar es salaam na wawasilishe vyeti halisi vya kuzaliwa na nakala zake. 

Pamoja na cheti cha kuzaliwa kwa kila mwamuzi ni lazima alete kadi ya kupigia kura au passport ya kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa umri wake.

Washiriki wa kozi watafanya mitihani ya kupima afya, utimamu wa mwili na sheria za mpira wa miguu Trivia (kuandika), video clips (offside na match analysis).

Waamuzi watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi arobaini (40) na
waamuzi wasaidizi sabini (70) watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
kwa msimu wa 2015/2016.  Shirikisho linawatakia wote maandalizi mema.

Baada ya kozi ya waamuzi kutakuwa na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ambayo itafanyika kuanzia tarehe 24/08/2015 hadi tarehe 25/08/2015.

Makamisaa wote wanatakiwa kuripoti tarehe 23/08/2015 saa 10:00 alasiri uwanja wa Taifa, Makamisaa watakao husika na kozi hii ni wale wote walio simamia michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2014/15.

Makamisaa watafanya mtihani wa sheria za mpira wa miguu (Trivia, offside, match analysis) na kupima mwamuzi anapochezesha (evaluation).  Wale watakaofaulu ndiyo watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: