Friday, July 10, 2015

HILI NDIYO TUKIO KUBWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Waumini wa Dini ya Kislam pamoja na wakristo nchini Tanzania  pamoja wapenda amani wote Tanzania na duniani leo wameungana na wapinga dhuluma nchini kote katikamatembezi ya aman ya kulaani dhuluma na uonevu mbalimbali wanaofanyiwa wanaadamu hususani mauaji yanayoendelea nchini palestina.

Matembezi hayo ya amani yamefanyika asubuhi ya leo Jijini Dar es salaam ya kuanzia msikiti wa kichangani uliopo magomeni jijini dare s salaam hadi kufika kigogo ambapo yamehudhuriwa na viongozi na waumini wa dini mbalimbali nchini Tanzania lengo likiwa ni kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa wanadamu nchini palestina na mataifa mengine ambayo unyama huo unafanyika.

Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA akigawa bendera za tanzania na palestina kama ishara ya kuanza rasmi kwa matembezi hayo lep jijini Dar es salaam,picha ya chini akizngumza na wahabari baada ya kumaliza matembezi hayo

Katika matembezi hayo mtandao huu ulipata nafasi ya kuhudhuria ambapo mwandishi wetu alizungumza na kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA ambaye amesema kuwa waumini wa dini pamoja na viongozi mbalimbali katika nchi ya Tanzania wanatakiwa kuliangalia taifa la palestina kwa jicho la tatu kama wanavyoliangalia taifa la Tanzania kutokana na kutengwa na mataifa mengine huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita vilivyodumu kwa muda mrefu sasa takribani miaka 67 .

Ameongeza kuwa kwa sasa ni wajibu wa kila kiongozi wa dini na wapinga dhuluma kote nchini kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinaendelea katika mataifa hayo ikiwemo taifa la palestina na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la palestina na Tanzania kwa dunia na historia yake kwa ujumla.

Amesema kuwa haki yoyote wanayodhulumiwa wapalestina haki hiyo wamedhulumiwa watanzania  waislam na wakristo na unyanganyi wowote wa ardhi wanaofanyiwa wapalestina haujafanywa kwa waislam tuu bali umefanywa kwa madhehebu na dini zote duniani hivyo ni lazima dunia iungane kuwatetea wapelestina hao

Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa leo siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ni siku ya ukombozi wa mwanadamu duniani kutoka katika uonevu,ukandamizaji,na unyanyasaji wa mwanadamu ambapo palestina ndio msikiti wa QUDS unakopatikana

Matembezi hayo yamewakutanisha waislam na wakristo pamoja na wapenda amani duniani kote yamefanyika leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo yameandaliwa na HAWZAT IMAM SWADIQ,pamoja na kamati ya Quds na Tanzania Itnasheriya Community(T.I.C).
PICHA NYINGINE NYINGI ZA TUKIO HILO ZIPO CHINI 















No comments: