Thursday, July 9, 2015

MANENO YOTE MUHIMU YA RAIS BUNGENI YAPO HAPA,KUMSHUKURU LOWASA,TIMU YA TAIFA,NA MENGINE



Rais Jakaya Kikwete akihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda.

FUATILIA MAMBO YALIVYOKUWA YANAKWENDA BUNGENI


Rais anaanza kuzungumza sasa; 
Kikwete: Mhe Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Hatimaye siku ya kulivunja Bunge imewadia. Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ya kulihutubia bunge ili kutimiza wajibu wangu huo wa kikatiba. Lakini shukrani yangu kubwa ni kwako kwa kuliongoza bunge hili kwa uhodari mkubwa.

Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari. Wewe ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika muhimili huu wa kutunga sheria. Na umethibitisha ya kuwa 'Wanawake wakipewa, wanaweza'.

Niwashukuru wabunge kwa kushiriki vema shughuli za bunge na mmelitendea haki na kuliletea heshima na hadhi.

Kikwete: Nilipofungua Bunge la tisa, nilisema; 'Tutatelekeza wajibu wetu kwa Ari mpya. Nguvu mpya na Kasi mpya'. Niitaja vipaumbele vya kufanyia kazi na ilipofika awamu ya pili, nikafungua Bunge la 10 kwa "Ari zaidi, Nguvu zaidi na kasi zaidi".

Kikwete: Tumekutana na changamoto nyingi sana kama taifa, ikiwemo dalili za chuki za kidini, lakini kupitia mazungumzo tumeweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa dini na wengineo.

Kikwete: Wanaozungumza hawagombani na humaliza tofauti zao bila kugombana

Kikwete: Nawashukuru wananchi wote kwa ushindi tulioupata kudumisha Umoja wa Nchi yetu; tahadhari ni muhimu bado.

Kikwete: Kama kura ya Maoni ingefanyika tukapata Katiba Mpya, tungekuwa hatuongelei kero kadhaa 

Kikwete: Nawashukuru wabunge kwa kuupitisha Muswada wa Gesi na Mafuta 

Kikwete: Mazingira ya Kisiasa visiwani Zanzibar yamekuwa bora kuliko awali kabla ya Muafaka kati ya CCM na CUF 

Kikwete: Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama. JWTZ imefanya kazi na Jeshi letu limeimarishwa nyanja zote

Kikwete: Jeshi letu lina utayari wa kivita kwa kiwango cha hali ya juu. Weledi umepanda kwa kiwango kikubwa Kikwete: Namaliza kipindi changu kama Amiri Jeshi Mkuu kwa kujiamini, kwamba tupo salama!

Kikwete: Mwaka 2005/2006 kulikuwa na matukio makubwa ya Ujambazi, niliahidi kupambana nao. Tumewadhibiti, hali ni tofauti sasa

Kikwete: Lazima tuendelee kutafuta muarobaini wa ajali za barabarani 

Kikwete: Changamoto kubwa iliyopo hadi sasa ni msongamano wa wafungwa magerezani 

Kikwete: Serikali imetimiza wajibu wake, Bunge limefanya kazi kubwa! 

Kikwete: Iwapo Katiba Pendekezwa itapita, nchi yetu itapata heshima kubwa sana

Kikwete: Tumeimarisha demokrasia, wanasiasa wanaandamana, wanatoka nje ya Bunge.

Kikwete: Habari kubwa nchini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu. Tarehe 25 Oktoba ni siku ya Uchaguzi; maandalizi yanaendelea

Kikwete: Tumefanikiwa sana kutoa Uhuru wa Vyombo vya Habari! Tuna magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Sani... 

Kikwete: There's no Media Censorship in Tanzania #PressFreedom

Kikwete: Nasikitika kuwa hatukuweza kupata Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Media Services Bill; wenzetu wajao watamalizia!

Kikwete: TAKUKURU imepewa meno ya kudhibiti na kupambana na Rushwa. Ina ofisi kila Mkoa na kila Wilaya 

Kikwete: Tumepata mafanikio makubwa, mapato ya Serikali yameongezeka. Bajeti ya Serikali imekuwa mara 5 ya mwaka 2005 ilivyokuwa


Kikwete: Tumepunguza utegemezi wa misaada katika Bajeti toka 42% hadi 8% kwa kusimamia ukusanyaji mapato



Kikwete: Sehemu kubwa ya Fedha za Serikali inaenda ktk Ununuzi wa Huduma; bila usimamizi mzuri wizi hutawala!

Kikwete: Nafurahi kuwa Taarifa za CAG zinapewa uzito mkubwa na hatua huchukuliwa. POAC/PAC imefanya kazi nzuri pia

Kikwete: Pale inapobainika kuna wizi, hatua za haraka kuwajibisha wahusika zinachukuliwa hata bila kusubiri kuwasilishwa Bungeni

Kikwete: Hati zimeongezeka Serikalini tokana na utendaji mzuri wa Ofisi ya CAG. Tuliajiri vijana wenye CPA km 780 hivi na kuwasambaza nchini


Kikwete: Ili shughuli zilizopangwa katika Bajeti ziweze kufanyika, inabidi Hazina itoe fedha kwa wakati



Kikwete: Tumeongeza Majaji wa Mahakama ya Rufani toka 8 hadi 16. Majaji wanawake wameongezeka toka 8 hadi 37!


Kikwete: Tunao majaji wakazi 1,266 na kati yao majaji wanawake ni 534 

Kikwete: Mrundikano wa kesi utakuwa historia katika muda mfupi ujao tokana na ongezeko la majaji na mahakimu

Kikwete: Ujenzi wa Mahakama kila Mkoa unaendelea katika Mikoa 9. Tunatenganisha kazi ya Upelelezi na Kushtaki 

Kikwete: Nimeamua kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe kwa kuugawa Mkoa wa Mbeya. Wilaya za Ubungo, Kigamboni zimeanzishwa 

Kikwete: Kila mwaka tumeongeza kima cha chini cha mshahara toka TZS 65,000/= (2006) hadi TZS 300,000/= (2015)

Kikwete: Idadi ya wabunge wanawake imeongezeka toka 62 hadi 127 sasa!

Kikwete: Vyuo vikuu kulikuwa na wanafunzi wa kike 10,000+ mwaka 2005 na sasa wamefikia 78,000+

Kikwete: Pato la Taifa limekua kwa 7%, Tanzania ni miongoni mwa mataifa 20 Duniani yenye uchumi unaokua kwa kasi 

Kikwete: IMF wanasema Pato la Tanzania ni kubwa kuliko walivyodhania. Tumebakiza kidogo sana kuingia kwenye Nchi za Pato la Kati 

Kikwete: Mauzo yetu nje (export) yameongezeka mara 7; mfumko wa bei si mkubwa

Kikwete: Tulianzisha BRN, tulianza na sekta 6; tukaongeza nyingine 3. Ni mpango wenye manufaa makubwa 

Kikwete: Tulianzisha PPP ili kuweza kurahisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi 

Kikwete: Tanzania inaongoza Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji mkubwa 

Kikwete: Tumepania kulirudisha jembe kwenye jumba la makumbusho, iwe historia

Kikwete: Sekta ya Kilimo nchini imekua kwa kiwango kinachoridhisha

Kikwete: Sekta ya Viwanda imekua ingawa bado jitihada zinahitajika kufanikisha zaidi

Kikwete: Uvuvi haramu umepungua ingawa haujaisha; mapato toka Sekta ya Uvuvi yameongezeka 

Kikwete: Sekta ya Utalii inachangia 25% ya mapato ya fedha za kigeni

Kikwete: Ajira zimeongezeka; tuna tishio kubwa la Ujangili hasa unaohusisha Meno ya Ndovu, tumefanya operesheni kadhaa

Kikwete: Viwanda vimeongezeka toka 15,000+ hadi 51,000+ sasa. Tunategemea ukuaji zaidi. Ujenzi wa Liganga/Mchuchuma unaanza mwezi ujao 

Sekta ya Madini ni ya 2 kuingiza fedha za kigeni. Tumefanya marekebisho ya mikataba ili itulinde sisi pia

Kikwete: Bei ya dhahabu ikipanda, sekta ya Madini itakuwa ya kwanza kuingiza fedha za kigeni

Kikwete: Migodi mipya 3 imeanzishwa katika miaka 10 iliyopita. Ajira ktk Sekta ya Madini imeongezeka toka 3,500 hadi 15,000+ 

Kikwete: Tumetenga maeneo 8 kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili wasisumbuliwe. Tumeanzisha mfuko wa kuwakopesha pia 

Kikwete: Vijiji 5,336 vimepatiwa umeme kwa mpango wa REA. Watanzania 40% wanapata umeme toka 10% ya 2006 

Kikwete: Tanzania inazo trillion 56.08 za akiba ya Gesi iliyogunduliwa; utafiti unaendelea. Inakadiriwa tunazo trillion 200 za gesi!

Kikwete: Nawashukuru sana Wabunge kwa kupitisha Miswada ya Gesi; ikifikishwa kwangu nasaini mara moja! 

Kikwete: Mtandao wa Barabara umeboreshwa; adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa Kanda ya Ziwa imekwisha

Kikwete: Tumeongeza bajeti ya barabara toka bilioni 73 mwaka 2005 hadi Bilioni 800+ sasa 

Kikwete: Vyombo vya Moto vimeongezeka toka 1,000,000+ hadi 3,000,000+ ingawa ongezeko hili limepelekea ongezeko la misongamano barabarani

Kikwete: Tutajenga Flyovers za TAZARA na Ubungo. Mpango wa kuendeleza Reli jijini Dar unaendelea

Kikwete: Tusipofufua Reli mapema, barabara hizi zitaharibika mapema sana 

Kikwete: Kuongezeka kwa mizigo inayopita Bandari zetu hadi sasa kunachangia 15% ya Pato la Taifa

Kikwete: Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Dar utakamilika October 2015. Ndege kubwa zaidi zitaanza kutua Dar

Kikwete: Watanzania wanaosafiri kwa ndege wameongezeka kwa sababu hali ya Maisha ni nzuri "Kidumu Chama Cha Mapinduzi jamani"; kumradhi

Kikwete: Feb 2015, TMA imepata ISO na taarifa zake zinatambulika na kukubalika kokote Duniani

Kikwete: Baada ya ujio wa mkongo wa intaneti; gharama za mawasiliano zimeshuka toka Sh. 115 hadi 36 kwa dakika 

Kikwete: Tanzania imepata ongezeko la watumiaji wa Intaneti toka watu milioni 1 kwa 2005 hadi milioni 12 mwaka 2015

Kikwete: Sekta ya nyumba imekua kwa kasi kubwa. Dar ya 2005 si sawa na ya 2015; NHC na NSSF wamewekeza kwa kiwango kikubwa pia

Kikwete: Nyumba za bati zimeongezeka; nyumba za nyasi zimepungua kwa kiasi kikubwa sana

Kikwete: Hakuna Taifa lililopata maendeleo bila kuendeleza Elimu. Tumetimiza ahadi 

Kikwete: Hakuna Taifa lililopata maendeleo bila kuendeleza Elimu. Tumetimiza ahadi 

Tumeendesha kampeni za malaria, tumegawa vyandarua milioni 26 mpaka wengine wanafugia kuku lakini matokeo yake tumepunguza maambukizi kwa asilimia 51 na tumepunguza vifo kwa asilimia 71. Sasa kuna huduma ya kupunguza maambukizi ya VVU mama kwenda kwa mtoto. Wauguzi sasa ni 22,942 na uwiano wa daktari kwa mgonjwa sasa ni 1:6600 na nesi 1:2340. Umri wa kuishi umetoka miaka 49 mpaka niaka 62 mpaka wafanyakazi wanauliza umri wa kustaafu unaweza kuongezeka?

Sekta ya maji tumevuka malengo japo bado ina matatizo makubwa sana hivyo lazima tuongeze uwekezaji na tumeongeza huduma ya uondoaji taka. Tumeongeza mifuko ya kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali wadogo, tumeiwezesha benki ya wanawake kuanza na asilimia 82 ya mikopo yote imetolewa kwa wanawake.

Tumetimiza ahadi ya kuimarisha ushirika nchini imeongezeka hadi mara tatu ya vyama vya ushirika vilivyokuwa awali. Niliahidi kusaidia kukuza michezo na sanaa ikiwemo kulipia makocha na nimetimiza. Netiboli na soka usiseme kila wakifukuza tunalipia mwingine, soka hatufanyi vizuri mpaka mimi naenda viwanjani. Nilifanya uamuzi wa kurejesha michezo mashuleni na matarajio yetu usoni yunaweza kufanya vizuri. Tunajenga kituo kwa ubia wa Symbion na Sunderland pale kidongo chekundu. Mwaka jana niligharamia timu ya wazoefu kutoka marekani kuja kutoa mafunzo kwa wasanii wetu wa filamu nchini.

Wasanii wa muziki tumelipia mastering studio, tumefanya jitihada kubwa ya kutunga kanuni za kulinda haki za wasanii, nitajitahidi katika kipindi kifupi kilichobaki kuyasukuma kwa nguvu, angalau tupate mahali pa kujiliwaza kutokana na soka kutofanya vizuri.

Tanzania ni rafiki wa kila nchi duniani, hadhi yetu katika uso imepanda sana. Marais wa China wametutembelea na kila mkubwa duniani ameshafika hapa pia tumeshirikishwa katika shughuli nyingi za kimataifa na nimekuwa mwenyekiti wa tume nyingi sana duniani. Katika kipindi hiki pia tumefungua balozi 5 na kuwa 35. Jumuiya ya EAC mambo yetu mazuri na mauzo yetu kwa jumuiya yameongezeka. Tumefanya mengi na kitabu mtapata, mtayasoma.

Namalizia sasa, tumefanya mengi lakini hatujayamaliza yote hata hivyo tumeweza kutekeleza asilimia 88 ya ahadi zilizomo katika ilani na za serikali. Niliulizwa unapenda watanzania wakukumbuke kwa lipi, Nilisema napenda wanikumbuke kuwa Rais Kikwete alitukuta kule na sasa ametuacha juu zaidi.

Nitakuwa mchoyo wa fadhili nisipowashukuru, makamu wa rais, rais wa Zanzibar Dk Ali Shein ambae pia alikuwa makamu wa rais, waziri mkuu Mizengo Pinda mpaka wakati mwingine, napenda kumtambua pia mheshimiwa Edward Lowassa katika kipindi alichokuwa waziri mkuu kafanya kazi nzuri, katibu mkuu kiongozi, wakuu wa wilaya na wengine wote waliofanikisha katika awamu hii ya nne, Nakishukuru chama changu, CCM kwa kuniamini, kuniunga mkono na kunisaidia kwa karibu kwa miaka yote kumi. Mwisho naishukuru sana familia yangu, namshukuru mke wangu Salma, unajuwa kule nyumbani ukiliwazwa unafanya kazi ya watu kwa uadilifu. Kila mwanaume mwenye mafanikio, mwanamke yuko nyuma yake.

Ninapowaaga wengine mnarudi kutetea majimbo yenu, nawatakia kila lakheri. Nawatakia kila laheri mlioamua kustaafu, nyio ndio wenzangu na mie. Mliotangaza nia nawatakia kila laheri, ila mko wengi, tuna kazi kubwa kuwapunguza mfikie watao ila msitununie tu. Nawapenda sana wananchi na nitaendelea kuwapenda mpaka Mungu atakaponiita.

Leo tunafanya utaratibu wa sherehe, kama harusi ni kitchen party mpaka tarehe 20 August 2015 nitakapotangaza rasmi ukomo wa bunge hili.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

No comments: