Saturday, July 11, 2015

SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM AUNGA MKONO KUPINGA YANAYOTOKEA HUKO PALESTINA


Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum  akizngumza katika semina hiyo leo jijini Dar es salaam
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watu wanaodhulumiwa na kuonewa katika mataifa mbalimbali hususani taifa la palestina ni jukumu la watu wa aina zote bila kujali dini,utaifa wala utofauti wowote uliopo.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na waislam wa dhehebu la shia kwa waialam pamoja na watu wote wanaopinga dhuluma na uonevu mbalimbali duniani,semina iliyofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waumini wa dini ya kiislam pamoja na dini zote na wapinga uonevu wote.
Baadhi ya waumini waliohudhuria semina hiyo
Semina hiyo ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya QUDS duniani siku ambayo ni maalum kwa watu wanaopinga dhuluma na kuthamini haki za binadamu ambapo katika maadhimisho hayo waumini hayo wameyatumia kutafakari na kukemea kwa pamoja kile ambacho kinaendelea katika taifa la palestina.
Baadhi ya picha ambazo zinaonyesha madhara ya vita inayoendelea nchini palestina 
Akizungumza katika semina hiyo mgeni rasmi ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa siku ya QUDS ni siku ya watu wote na madhehebu na dini zote na sio siku ya wapalestina pekee kwa sababu ni siku ambayo inatumika kupinga kwa sauti moja uonevu wowote ambao unaendelea katika mataifa mbalimbali duniani.
Amesema kuwa sisi kama Taifa la Tanzania ni siku muhimu ya kutafakari amani ya dunia ikiwa ni pamoja na kupinga kwa sauti moja dhuluma yoyote inayoendelea dhidi ya watu wa palestina na mataifa mengine duniani.
Waumini hao wameanza kuadhimisha siku hiyo jana ambapo walifanya matembezi ya amani katika jiji La Dar es salaam kuwakumbusha watanzania juu ya kuiombea na kuisaidia nchi ya pelestina kutoka katika machafuko ambayo yanazidi kugharimu maisha ya watu

No comments: