Friday, July 10, 2015

VIDEO NA PICHA,KAULI ZA CCM ZINAVYOPISHANA,NAPE ASEMA MAJINA HAYAJATAJWA HADI ASUBUHI


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiongea na waaandishi wa habari mara baada ya kutoka kikao cha Kamati kuu.
Mhe. Emmanuel Nchimbi akitangaza mbele ya wanahabari kutangaza kutoridhishwa na maamuzi yao.
Mama Sophia Simba akizongwa na wanahabari  juu ya Kamati Kuu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA.

Hali si hali ndani ya Makao Makuu baada ya wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu uliomalizika usiku huu kushindwa kufikia maamuzi ya 5 bora na baadae 3 bora.

Kutoelewana huko kumetokana na wajumbe wakati wa Kamati Kuu ilichokuwa ikiendeshwa na Mwenyetiki wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kushindwa kuazimia maamuzi yaliyokuwa yameletwa.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho

 Nape, alisema kila kitu kitajulikana asubuhi ya Julai 12, 2015 huku wajumbe wwatau wa Kamati hiyo, Mhe. Nchimbi, Adamu Kimbisa na Sophia Simba kukataa maamuzi hao.

Mhe. Nchimbi akiongea na waandishi alisema wao wamekataa kuafiki kwa vile wamekiuka kanuni kwa kuleta majina machache ili yaweze kijadiliwa jambo ambalo si sawa.

No comments: