|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akirejesha fomu za wadhamini kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajabu Luhavi, jana, baada ya kukamilisha kazi ya kuomba udhamini kwa mikoa yote nchini. |
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU AMEREJESHA FOMU ZA WADHAMINI ALIOWAPATA KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI AMBAZO AMEZIWASILISHA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA NA AMESISITIZA UMUHIMU WA WANANCCM KUMUUNGA MKONO MGOMBEA YEYOTE ATAKAETEULIWA NA VIKAO VYA MAAMUZI NA KUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.
WAZIRI NYALANDU AKIONGEA BAADA YA KUKABIDHI FOMU HIZO KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM RAJABU LUHWAVI, AMESEMA HATUIA YA KUUNGANA WANACCM WOTE BAADA YA KUPATIKANA KWA MGOMBEA MMOJA ITAKIWEZESHA CHAMA KUIMARIKA NA AMESISITIZA UMUHIMU WA KUENDELEZA MISINGI YA UMOJA NA MSHIKAMANO ILIYOACHWA NA WATANGULIZI WA NAFASI YA URAIS AKIWEMO BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
|
MKE wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhavi ofisini kwake katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati Nyalandu aliporejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais. |
|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi. Kulia ni mkewe Faraja na kushoto ni Luhavi. |
|
BAADHI ya wanachama wa CCM waliomsindikiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma, jana. |
|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakipongezwa na sehemu ya umati uliojitokeza kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati akirejesha fomu. |
|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakisindikizwa na wanachama na maofisa wa CCM Makao Makuu Dodoma kwenda kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhavi, wakati walipofika kurejesha fomu za urais. |
|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakishangiliwa na mamia ya wanachama wakati wakiondoka ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, jana baada ya kurejesha fomu za kuomba urais. |
No comments:
Post a Comment