MWANAMUZIKI
wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania mwenye asili ya
kitaliano Christian Revbaer 'Muzmamoyo' amesema kuwa
bajeti nzuri walizonazo wanamuziki wa kimataifa
akiwemo Sean
Comb 'P Didy' ndiyo sababu zinazowafanya
waonekane bora
hivyo yupo radhi kutumia fedha nyingi ili
kufikia kiwango cha
kimataifa.
Hayo ameyasema
leo alipokuwa akizungumza
na Mwandishi
wa Habari24 blog Dar es salaam aliyetaka kujua mpango wan mwanamuziki huyo ambapo amemueleza
kuwa yupo radhi kuwekeza pesa nyingi ili kufanya kazi yenye ubora.
Amesema kuwa kuna haja ya wadhamini nchini zikiwepo kampuni za vinywaji
pamoja na makampuni ya simu kuwekeza fedha za kutosha katika tasnia ya muziki
kwa kuwa ni eneo linalotoa ajira nyingi
kwa vijana wa sasa badala ya kutazama tu mpira wa miguu.
Hata hivyo ameongeza kuwa mpaka sasa ni muzik pekee ndio anayeipeperusha
bendera bendera ya Tanzania katika mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment