Monday, August 17, 2015

Breaking newzz--Mgombea urais ACT agoma kugombea,hali sasa iko hivi hapa



Sakata la nani atapeperusha bendera ya urais kupitia cha cha ACT wazalendo liemechukua sura moya baada ya mgombea aliyepitishwa na kamati kuu ya chama hicho profesa KITILA MKUMBO kugoma kugombea nafasi hiyo kwa sababu alizosema kuwa hakujiandaa kisaikologia.


Mapema leo ndani ya tume ya taifa ya uchaguzi katibu mkuu wa chama hicho SAMSON MWIGAMBA alichukua form ya kugombea urais kwa kumuwakilisha kitila mkumbo ambapo akizngumza na wanahjabari alisema kuwa tayari kamati kuu ya chama hoicho kwa kauli moja imekubaliana kumsimamisha mgombea huyo kuwania nafasi ya u8rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Baada ya kuchukua form hiyo kitila mkumbo kupitia mitandao mbalimbali ya habari aliamua kutoa tamko la kutokuwa tayari kuwania nafasi hiyo kwa sababu za kutokujiandaa kikamilifu katika kuwania urais kauli ambayo imeanza kupingwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho huku wengi wakimtaka kugombea nafasi ya urais wa chama hicho.

Ndani ya makao makuu ya chama hicho mchana wa leo mtandao huu umeshughudia baadhi ya wananchi ambao ni wanachama wa chama hicho wakiandamana kupinga kauli ya kitila mkumbo ya kutotaka kugombea nafasi hiyo huku wengi wakimtaka kubadilisha dhamira yake na kugombea nafasi hiyo.

Hadi sasa viongozi wa chama hicho wameingia tena kwenye kikao kipya na kitila mkumbo kumbembeleza akubali kugombea nafasi hiyo.


TAMKO LA KITILA MKUMBO MAPEMA LEO


Kitila Mkumbo

5 mins · 

Ndugu Wazalendo,
Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili.


Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.


Baada ya tafakari na mawasiliano (consultations) mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu.


Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu lakini naamini kwamba mtaheshimu uamuzi wangu na kwamba hamtaacha kuthamini mchango wangu katika chama kwa sababu ya kukataa kugombea urais.


Nasikitika kwa tuhuma ambazo baadhi ya wanachama wetu wanarusha katika mitandao ya kijamii na sehemu zingine. Nathamini na kuheshimu haki ya wanachama wetu kuonyesha hasira kwa jambo wasilolipenda. Hata hivyo nawasihi wanachama wetu wajizuie kuzusha mambo yatakayochochea chuki ndani ya chama na kukatishana tamaa.


Nashauri tuwaombe wanachama wetu wengine waandamizi wachukue jukumu hili, wakiwemo mama mwenyekiti na Katibu Mkuu, kuwataja tu kwa uchache.


Tunapotafari haya, tusisahau Malengo Mapana ya chama chetu tuliyojiwekea katika uchaguzi huu. Ni bahati nzuri kwamba tumefanikiwa kuweka wagombea wa ubunge na Udiwani katika kata na katika majimbo mengi. Tusiyumbe.


Ahsanteni.

Kitila Mkumbo

No comments: