Leo asubuhi nchini Tanzania kumeamka na story zilizokuwa zinaelezea kuwa chama cha CCCR MAGEUZI kitajitoa katika umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA kwa kile ambacho wameleza kuwa ni udicteta wa baadhi ya vyama hivyo.
Habari iliyoandikwa na gazeti la UHURU ambalo linamilikiwa na chama cha mapinduzi zilimnukuu mmoja wa viongozi wakubwa wa chama hicho FAUSTINE SUNGURA akisema kuwa leo chama hicho kitatangaza maamuzi magumu ya kujitoa ndani ya umoja huo.
Katika mkutano wa wanahabari muda mfupi uliopita ndani ya makao makuu ya NCCR amezngumza kaimu katibu mkuu mama NDELAKINDO KESSY (Pichani) amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa hakuna taarifa wala ukweli wowote wa jambo hilo pamoja na kusema kuwa mkurugenzi aliyetoa Taarifa hizo hajulikani alipo na sio msemaji wa chama hicho.
Aidha amesema kuwa mambo yanayohusu chama hicho msemaji mkuu ni mwenyekiti wa chama hicho JAMES MBATIA,huku akisema kuwa chama hicho kipo imara ndani ya umoja huo na hawawezi kujitoa huku akisema kuwa wanafanya utafiti wa kina kujua aliyetunga hiyo habari ili hatua zichukuliwe.
Hata hivyo majibu ya kiongozi huyo hayajaridhisha na Tayari mwenyekiti wa chama hicho JAMES MBATIA atawasili hapa makao makuu ya NCCR kuzngumza Tena na wanahabari ambao wanataka kujua ukweli wa jambo hilo sasa .
MTANDAO HUU UTAKUPA KILA KITU
No comments:
Post a Comment