Monday, August 31, 2015

DR. MAGUFULI AITIKISA SONGEA, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA

????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa  anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi  na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Amesema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Amesema ataongeza zaidi  kasi yake katika utendaji  tofauti na alipokuwa  Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa  akichaguliwa na watanzania kuwa rais  yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea  na kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki  miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumba ni kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SONGEA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.

????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akishuka kutoka katika kivuko cha Mv Lituhi mara baada ya kuvuka mto Luhuhu akitokea mkoani Njombe wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni zake.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipunga mkono mara baada ya kuvuka mto Luhuhu akielekea Mbinga mkoani Ruvuma.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mmoja wa wana CCM akifuta vumbi kwenye picha ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi mjini Mbinga kwenye uwanja wa Taifa kumsikiliza Dr John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Kada wa CCM Bw. Amon Mpanju akiwahutubia wakazi wa mjini Songea mkoani Ruvuma leo.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita.
????????????????????????????????????
Mabasi Maalum ya Kampeni za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa CCM jimbo la Songa Mjini Mh. Leonidas Gama.
14
Baadhi ya wana CCM wa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa CCM kwenye uwanja wa Taifa uliofanyika katika mji huo. 
15
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga.
16
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshika picha za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
K17
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Mbinga Komredi Sixtus Mapunda wakati alipokuwa akiwaomba kura wananchi wa mji wa Mbinga.
18
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi Mh. Jenista Mhagama mgombea ubunge wa jimbo la Peramiho katika mkutano uliofanyika Peramiho.
19
Wana Peramiho wakimkaribisha Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
20
22
Peramiho ikizizima kwa bendra za CCM wakati wa mapokezi hayo.
23
Umati uliohudhuria katika mkutano huo
24
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma.
25
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi mwenye ulemavu wa  ngozi mara baada ya kumaliza mkutano wake uliofanyika Peramiho.
26
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mh.Jenista Mhagama ambaye Mgombea ubunge wa jimbo la Peramiho 
27
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa na watoto mara baada ya kumaliza mkutano wake Peramiho.
28
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.
29
Majimaji ikiwa imetapika
30
Kundi la TOT likifanya vitu vyake jukwaani.
31
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali wakiwa wameketi meza kuu.
33
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Songea mjini Dr. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi na kumpigia debeMgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea. 
34
Huyu naye alivaa makufuli kichwani na shingoni kupeleka ujumbe wa mapenzi yake kwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
35
Kutoka kulia ni Mwingulu Nchema, Jenista Mhagama na William Lukuvi wakiteta jambo.
36
Mgombea Ubunge wa jimbo la Songea mjini Mh. Leonidas gama akijinadi kwa wananchi kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
37
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji

No comments: