Thursday, August 13, 2015

KAMANDA KOVA CUP YAZINDILIWA DAR MUDA HUU

Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mama SOPHIA MJEMA akikabidhi kombe kwa kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Jijini Dar es salaam mapema leo 
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo limezindua rasmi mashindano ya michezo mbalimbali yatakayoendeshwa jijini Dar es salaam ambayo yatashirikisha michezo yote,michezo ambayo inalengo la kuwashirikisha wananchi wa rika na itikadi mbalimbali mashindano yaliyopewa jina la KAMISHNA KOVA CUP.

Akifungua mashindano hayo mkuu wa wilaya ya temeke ambaye kwa sasa ni kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mama SOPHIA MJEMA amesema kuwa mashindano hayo yamekuja kipindi kizuri ambacho Tanzania inajiandaa na uchaguzi mkuu ambapo amesema kuwa ni vyema mashindano hayo yatumike kuwaunganisha vijana na kuilinda amani na upendo uliopo Tanzania.
Kukata utepe
Mama Sophia amesema kuwa kipindi cha uchaguzi ni nkipindi ambacho vijana ambao hawana shughuli maalum wamekuwa wakirubuniwa na watu ambao hawaitakii mema Tanzania kwa kuwapa hela ili wafanye lolota ili kuivuruga amani ya nchi jambo ambalo amesema mashindano hayo yamekuja kuhakikisha kuwa vijana wanashitriki na kuacha kukaa bila kitu cha kufanya na kuwafanya kujiepusha na makundi ya uvunjifu wa amani.
Naye mhasisi wa mashindano hayo ambaye ni kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam ASP SULEMAN KOVA amesema kuwa kupotia mashindano hayo jamii itafaidika kupata elimu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi,matumizi ya aina mbalimbali ya madawa ya kulevya,wizi katika mitandao,uzururaji,na kukaa katika vijiwe bila kazi.Pamoja na kujenga na kuimarisha ushirikiano baina ya jamii na jeshi la polisi.


Katika mashindano hayo ambayo yanataraji kumalizika mwezi wa 11 baadhi ya zawadi kwa washindi ni pamoja na vikombe,vyeti vya ushiriki na Fedha Taslim.

Wadau mbalimbali ambao wanashiriki katika mashindano hayo yaliyozinduliwa Jijini Dar es salaam

No comments: