Friday, August 28, 2015

Kauli za Rais MKAPA sasa zaibua mengine,TACCEO waibuka na kusema haya

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ambao ndio waratibu wa mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi Tanzania TACCEO akizngumza na wanahabari kwa niaba ya mwenyekiti wa mtandao huo mapema leo jijini Dar es sakaam kuhusu uhakiki wa majina ya daftari la kudumu la wapiga kura na mwenendo wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania
 Ikiwa ni siku chache Tangu Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh BENJAMIN MKAPA  kutoa kauli ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kuwa ni lugha chafu, sakata hilo limeanza kuchukua sura mpya baada ya wadau mbalimbali kuanza kujitokeza kulaani na kupinga matumizi ya lugha kama hizo katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.

Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO wamekuwa wa kwanza kuibuka na kulaani vikali vitendo hivyo ambavyo wamedai kama tume ya uchaguzi na vyombo husika vitafumbia macho vinaweza kusababisha machafuko na chuki kwa watanzania.

Akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam HELLEN KIJO BISIMBA kwa niaba ya nmwenyekiti wa TACCEO amesema kuwa matumizi ya lugha za kejeli,dharau,na vijembe katika kampeni yataleta chuki na hatimaye kupelekea uvunjifu wa amani jambo ambalo lazima wanasiasa wawe makini wanapokuwa majukwaani kuepuka kuwagawa watanzania na kuwapandikiza chuki.
Baadhi ya wanabari wakichukua Taarifa hiyo
Akitolea mfano kauli aliyoitoa Mh MKAPA katika viwanja vya jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi siku ya jumapili ambapo alisema kuwa watanzania ambao wanataka ukombozi wa Tanzania huku wakijua kuwa nchi tayari ilishakombolewa miaka mingi iliyopita ni upumbavu na ulofa wa watanzania hao.Bi BISIMBA amesema kuwa kauli kama hizo hazikutakiwa kutolewa mbele ya watanzania wenye mawazo na mihemuko ya kisiasa na ilitakiwa lugha hizo kukemewa mara moja na mamlaka husika lakini cha kushangaza hakuna mtu aliyejitokeza kulaani vitendo hivyo.

Aidha akizungumzia mambo yanayoendelea katika mitaa mbalimbali ya kuzomea watu wenye sare ya chama tofauti na itikadi zao TACCEO wamesema kuwa tabia hiyo kama ikiachwa bila kukemewa kwa lugha moja inaweza kuhatarisha amani ya Tanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kwani inajenga hasira kwa wale wanaofanyiwa vitendo hivyo na baadae kuamua kufanya fujo.

Mtandao huo ambao leo ulikuwa unatoa Taarifa kuhusu uhakikiki wa majina katika daftari la kudumu la mpiga kura na mwenendo wa kampeni za uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani wameelezea mambo kadhaa waliyoyabaini katika mazoezi hayo.

Katika zoezi la uhakiki wa Daftari la kudumu la wapiga kura wamesema kuwa mchakato huo umegubikwa na kasoro kadhaa ambazo wamezitaja kuwa ni kukosekana kwa taarifa sahihi za zoezi zima la uhakiki wa majina ya waliojiandikisha,kukosekana kwa majina kwa baadhi ya wananchi waliojiandikisha,majina kuonekana sehemu tofauti na ile waliyojiandikisha pamoja na changamoto nyingi ambazo wameitaka tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa wanazitizama mara moja kabla ya uchaguzi mkuu.

No comments: