Friday, August 28, 2015

Nimekuwekea mambo muhimu aliyoyazungumza ZITTO KABWE leo Jijini Dar es salaam

Mh ZITTO KABWE kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo akionyesha bango la mgombea ubunge jimbo la kongwe ambaye anadaiwa kuanza kusambaza mabango ya kampeni kabla ya muda husika na tume ya uchaguzi kuliacha swala hilo licha ya malalamiko kadhaa kutoka kwa wapinzani 

 Chama cha ACT wazelendo leo kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa sasa.

Kiongozi mkuu wa chama hicho ZITTO ZUBER KABWE akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo amesema kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania kilichodiriki kuwapa mafunzo ya kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa wanakwenda na lugha moja kwa watanzania kueleza mipango na ilani ya chama hicho.
ZITTO KABWE akiendelea kutoa mafunzo kwa wagombea ubunge zaidi ya 90 walioshiriki katika mafunzo hayo
ZITTO KABWE anasema kuwa chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee nchini Tanzania ambacho kina agenda maalum kwa watanzania tofauti na vyama vingine ambavyo amesema kuwa vinatumia mbwembwe na ulaghai kwa watanzania bila kuweka wazi nini wanataka kuwafanyia watanzania.

Amesma kuwa mambo ambayo chama hicho kimekuwa kikiyapigania na kitaendelea kuyapigania ni pamoja na mambo ya hifadhi ya jamii kuhakikisha kuwa watanzania wote wanafaidika nayo,pamoja na miiko ya uongozi na kukemea ufisadi kwa nguvu moja ambapo amesema kuwa kwa sasa hakuna chama hata kimoja kinazubutu kusimama na kukemea ufisadi kwani nao wamekuwa sehemu ya ufisadi huo.

HIZI NDIO HISTORIA ZILIZOWEKWA NA ACT HADI SASA KUELEA UCHAGUZI MKUU.

Akizungumza Mh ZITTO KABWE amesema kuwa kikiwa ni mara ya kwanza kushiriki katika uchaguzi mkuu chama cha ACT WAZALENDO kimeweza kusimamisha wagombea ubunge katika majimbo 219 kati ya majimbo 265 jambo ambalo linakifanya chama hicho kuwa ni chama cha pili kwa wagombea ubunge wengi huku cha kwanza kikiwa ni chama cha mapinduzi CCM.

Historia nyingine ambayo chama hicho kimeiweka ni kuweza kusimamisha wagombea ubunge wanawake wengi kuliko vyama vingine vyote nchini Tanzania ambapo chama hicho kimesimamisha wanawake 25% sawa na wabunge 55 katika majimbo toifauti tofauti nchini Tanzania huku kubwa ni kusimamisha mgombea urais mwanamke.

Historia nyingine ni hii chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee kilichosimamisha wagombea wenye umri mdogo kuliko vyama vyote nchini ambapo mgombea mwenye umri mdogo ana miaka 21 na mwingine akiwa na miaka 23 ambapo amesema kuwa ni ishara kuwa chama hicho kinawajali vijana.

Mh ZITTO akizungumzia changamoto ambazo chama hicho kinakumbana nazo amesema kuwa hujuma mbalimbali kutoka kwa wapinzani wao zimekuwa nyingi ikiwemo kukatwa kwa majina kadhaa ya wagombea wao bila sababu za msingi mfano jimbo la kinondoni ambalo msanii KALAPINA alikatwa katika orodha ya wagombea bila kutolewa sababu jambo ambalo limewafanya kukata rufaa.

Amesema kuwa hujuma hizo sio mwaka huu zimeanza ni kila mwaka huwa zinatokea kutokana na vyama vingine hususani chama cha mapinduzi kuishiwa na mbinu za ushindi na kuanza kuwahujumu wapinzani,ambapo amesema kuwa wao kama ACT WAZALENDO wataendelea kupigana hadi hatua ya mwisho.
Chama hicho kitazindua kampeni zake siku ya jumapili katika viwanja vya zakiem mbagala Jijini Dar es salaam ambapo wanataraji kuweka wazi mipango na ilani ya chama hicho.

No comments: