Wednesday, August 19, 2015

KUZIONA AZAM NA YANGA ELFU 7,000/=


Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni silingi elfu saba..

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangaza viingilio vya mchezo huo ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni, kuwa ni tsh 7,000 kwa majukaa yenye rangi ya kijani, bluu na rangi ya chingwa, VIP B & C tsh 20,000 na VIP A tsh 30,000.
 Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo jumamosi asubuhi saa 2 kamili katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Mchezo huo wa Ngao ya Jamii utachezeshwa  na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo, (Dsm), akisaidiwa na Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Josephat Daud Bulali (Tanga), mwamuzi wa akiba Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.

No comments: