Baada ya Magazeti kadhaa leo kuandika habari kuwa chama cha Democrasia na maendeleo chadema kimepanga kuzindulia kampeni zake za uchaguzi katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam hatimaye serikali imeibuka na kupiga marufuku matumizi ya uwanja huo kwa kile walichosema kuwa sio matumizi ya uwanja huo.
Akizungumza na wanahabari muda huu Jijini Mkurugenzi wa idara ya Habari maelezo Bwana ASSA MWAMBENE (pichani) Amesema kuwa ni kweli walipokea maombi kutoka CHADEMA tarehe 12 mwezi wa nane ya kuomba kutumia uwanja wa taifa mpya kwa ajili ya kuzindua kampeni na Tayari wameshawajibu kuwa hawawezi kuruhusu uwanja wa serikali kutumika kwa shughuli za kisiasa kwa chama chochote nchini.
Amesema kuwa wameshangaa kuona Taarifa mbalimbali kwenye magazeti leo zikisema kuwa kampeni ya CHADEMA itazinduliwa hapo wakati tayari serikali imeshapiga marufuku sehemu za serikali kutumika katika shughuli za kisiasa.
|
No comments:
Post a Comment