Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadam LHRC akizngumza na wanahabari leo juu ya maswala ya Maadili kwa viongozi kuelekea uchaguzi mkuu. |
Kituo cha sheria na
haki za Binadamu nchini Tanzania kimeitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi
kutokupitisha majijna ya wagombea wa vyama mbalimbali ambao tayari
wameshausishwa na maswala mbalimbali ya ukiukaji wa maadili ikiwemo Tuhuma
mbalimbali za ufisadi, rushwa,pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.
Akizunguimza na
wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama
HELLEN KIJO BISIMA amesema kuwa katika kipindi hiki imeshughudiwa vyama vya
siasa vikiwapitisha viongozi kuwania nyadhifa mblaimbali za uongozi huku kukiwa
na viashiria vya kutoheshimu misingi ya maadili huku baadhi ya walioteuliwa wakiwa
wamewahi kuhusishwa na kutajwa na kushtakiwa katika vyombo vya kikatiba
kutokana na ukosefu wa maadili ya uongozi.
Amesema kuwa baadhi ya
wagombea ambao wamepitishwa na vyama mbalimbali vya siasa waliwahi kuhusishwa
na rushwa,matumizi mabaya ya ofisi za umma,kutowajibika,huku wengine wakiwa
waliwahi kutoa kauli za kejeli zinazokinzana na kanuni za maadili ya uongozi
huku wengine wakienda mbali zaidi na na kuvidharau vyombo vilivyowekwa kikatiba
kusimamia maadili ya umma.
Ameongeza kuwa kutokana
na viashiria hivyo ambavyo mwisho wake vinaweza kutupatia viongozi wasio na
maadili ni lazima vyombo vinavyosimamia maaadili,ya viongozi wa umma kutathmini
kwa makini,na kutofumbia macho viongozi wa umma ambao wanawania tena nyadhifa
mbalimbali ambao walishindwa kuonyesha kiwango cha juu cha maadili wakati wa
uongozi wao,ili wananchi wawe na imani nao kwa mara nyingine.
Katika hatua nyingine
mkuruhenzi huyo ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania
kwa kuzingatia sheria ya kupambana na kudhibiti rushwa na sheria ya gharama za
uchaguzi iweke na kusimamia mkakati ambao utadhibiti mianya ya rushwa na
matumizi yasiyo halali ya nafasi na vyombo vya Umma katika kampeni za uchaguzi
mkuu.
No comments:
Post a Comment