Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania. Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera. Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati. Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia. Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT . Alizaliwa Oktoba 1959 Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge. Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu. Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu. Alianza siasa mwaka 1995 Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa. Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi. Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa. |
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond kutokana nauzembe wa watendaji walio chini yake.Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza
katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi.
Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015.Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:
Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)Mbunge wa Monduli tangu 1990
|
MACMILLAN LYIMO (TLP):
Macmillan Elifatio Lyimo alizaliwa tarehe 29 Januari 1964 katika kijiji cha Kondeni Matala wilaya ya Moshi Vijijini, katika jimbo la Vunjo, akiwa ni mtoto wa nne kati ya watoto sita wa familia ya mwalimu Elifatio Lyimo na mama Elingisongoya (Ametimiza miaka 51 mwezi Januari 2015).
Alianza elimu yake ya msingi katika shule za msingi Kondeni na Kirua kati ya mwaka 1975 na 1978 (darasa la kwanza hadi la nne). Kisha, mwaka 1978 hadi 1979 alisoma katika Shule ya Msingi Sanya Juu katika wilaya ya Hai . Baadaye alijiunga na Shule ya Msingi Karoro kati ya mwaka 1980 – 1981 alikomalizia darasa la saba.
Macmillan alikuwa mwanafunzi pekee aliyefaulu kutoka kwenye shule zote za kata ya Mwika kusini. Baada ya ufaulu huo wa “upweke” alichaguliwa kuendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Same mkoani Kilimanjaro akafanikiwa kuhitimu mwaka 1985.
Katika uhitimu wake wa kidato cha nne alipata Daraja la Kwanza (Division I) akachaguliwa tena kuendelea na masomo ya juu ya sekondari katika mchepuo wa ECA (Economics, Commerce na Accounts). Masomo haya ya juu ya sekondari (kidato cha tano na cha sita) aliyapata katika Shule ya Sekondari Umbwe iliyoko Moshi Vijijini (1985 - 1988) ambako nako alipata daraja la kwanza (Division I).
Baada ya hapo alijiunga na jeshi la kujenga Taifa katika kambi za Mgambo na baadaye Maramba zote zikiwa mkoani Tanga, kisha akahamishiwa makao makuu ya JKT eneo la Mlalakuwa jijini Dar es salaam, (Mwaka 1988 - 1989).
Na kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanzia mwaka 1989 na akahitimu shahada ya Biashara (Bcom) mwaka 1993. Katika kujiendeleza kitaaluma, Macmillan alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) mwaka 1999 – 2004 alikosoma na kutunukiwa shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA). Tangu mwaka 2013 amekuwa akiendelea na masomo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Huria Tanzania na hivi sasa yuko katika hatua ya utafiti akitarajia kuhitimu shahada hiyo ya falsafa miaka michache ijayo.
Tangu ahitimu shahada yake ya Biashara, Macmillan hajawahi kuajiriwa serikalini na haamini katika “kuajiriwa na serikali”. Amefanya shughuli za biashara ndogo ndogo kabla ya kufungua kampuni yake binafsi inayojihusisha na masuala ya madini na raslimali za Nchi.
Amejishughulisha sana na utafiti juu ya utajiri wa madini katika nchi hii pamoja na raslimali zingine. Lyimo amenieleza kuwa, Utafiti huu wa zaidi ya miaka 15 umemwezesha kujua ni kwa kiasi gani taifa hili ni tajiri katika eneo la madini,mafuta , gesi, ardhi, maji, mito na maziwa.
Ndoto yake kubwa ni kuona namna gani taifa linaweza kunufaishwa na rasilimali zake. Muda mfupi nilioongea nae tayari alishanipa vionjo vya kampeni yake mwezi oktoba mwaka huu vikiongozwa na kauli mbiu “FUTA UMASIKINI TANZANIA”!
Macmillan ni mwandishi mzuri wa vitabu na kitabu alichokikamilisha hivi karibuni kikiwa na kurasa zaidi ya 200 kinaitwa “Nuru ya Mabadiliko Tanzania kutokea mwaka 2005” ambacho kiko kwenye hatua za uchapishwaji.
Mwanasiasa huyu hapendi kuongea masuala yake ya kifamilia kwa hiyo sikupata taarifa za hali ya ndoa yake.
|
Chifu Lutalosa Yemba (ADC) ni mgombea wa chama hicho chenya maskani yake Buguruni jijini Dar es salaam,YEMBA pia alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Shinyanga .kabla ya kutimuliwa ndani ya chama hicho mapema mwaka huu na kujiunga na chama cha ADC na sasa ndiye mgombea urais wa chama hicho |
No comments:
Post a Comment