Friday, August 21, 2015

Mariado wanyakua ubingwa Airtel Rising Stars

 Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Adam Brown akikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa timu ya Mariado Munira Goda baada ya timu yake kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, jana jijini Arusha
Timu ya Mariado wakishangalia ubingwa kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka mabingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, Agosti 20 jana Arusha,


Na mwandishi wetu.
Timu ya wasichana ya Mariado imefanikiwa kunyakua ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stas mkoa wa Arusha. Mariado iliibamiza Crisking 3 – 0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Meru.

Timu zote zilianza kwa kasi lakini kadri muda ulivyozidi kwenda Crisking walipoteza umakini na kuwapa nafasi wapinzani wao kushinda mchezo huo. Mariado walipata magoli kupitia kwa Mariam Rashid aliefunga magoli mawili na Caroline Antipace alietimisha kwa kufunga goli la siku. 

Akiongea katika sherehe za kufunga katibu wa chama cha mpira wa miguu Adam Brown aliipongeza timu ya wasichana ya Mariado kwa kuchukua ubingwa na kuwataka kufanya juhudi zaidi. “ huu ni mwanzo tu katika  kazi yenu na mnapaswa kuongeza juhudi ili ndoto zenu zitimie za kua wachezaji nyota”, said Brown.   

Amepongeza wadhamini wa mashindano kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango katika mpira wa miguu Tanzania. “Mpira unaihitaji fedha ili uweze kuendelea. Tunashukuru sana kwa msaada wa fedha ambao tunaupata kutoka Airtel Tanzania katika kuendesha programu hii kwa vijana”, alisema 

Kumalizika kwa michuano hii ngazi ya mkoa inatuleta karibu na fainali za taifa zitakazo fanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar-es-Salaam kuanzia September 11 mpaka 21. Timu ya kombaini ya Arusha itashiriki michuanao ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa pamoja na timu za Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya na Mwanza.

Timu za wavulana zinashirikisha Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Mbeya na Mwanza. “Naamini vipaji vinavyozalishwa na Airtel Rising Stars kila mwaka vitalipeleka taifa hili katika Mafanikio makubwa,” Alisema Brouwn.

Speaking at the same occasion, Airtel representative Nassoro Laizer thanked officials of Arusha football association for their time and support of the tournament and underlined Airtel’s commitment to continue sponsoring this talent scouting football program.

Akizungumza katika hafla hiy0 muwakilishi wa Airtel Nassoro Laizer aliwashukuru viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa Arusha kwa muda wao na kushiriki kikamilifu katika mashindano na kusisitiza kuendelea kudhamini program hii ya kusaka vipaji.

Aliwataka wachzaji wa timu za wasichana kutumia vizuri fursa hii ya Airtel Rising Stars ili waweze kutimiza ndoto zao katika soka. 

No comments: