Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amepanga kujibu tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake ikiwemo kuitwa mshenga na Dk Wilbroad Slaa wakati akitangaza kujiuzulu wiki iliyopita.
Aidha, katika hotuba yake kwa Waandishi wa Habari Dr. Slaa alisema kwamba Gwajima alikuwa mshenga wakati wa kumkaribisha Edward Lowassa ndani ya Chadema ili awe mgombea urais.
Akizungumza wakati akihubiri katika kanisa lake ambapo baadhi ya waumini na wananchi walitarajia Askofu huyo angejibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na katibu huyo wa Chadema hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kanisani kwa kuwa kanisa sio mahala pa kuzumzia mambo ya siasa.
“Leo sitazungumzia masuala hayo hapa kwa kuwa hili sio pango la wanyang’anyi ila nitazungumza na vyombo vya habari Jumanne ijayo,” alisema.
Amesema kesho yaani jumanne atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjibu Dk Slaa ambaye amejitokeza mara mbili kutoa tuhuma hizo na kuwataka wajitokeze kumjibu kama wana hoja
No comments:
Post a Comment