Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Monica Laurent (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha msemaji wa mkutano huo kuzungumza na waandishi.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo ninastahili kushiriki uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mwanahabari wa gazeti la Nipashe, Theresia akiwa mbele ya kamera wakati wa mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania kimetoa onyo kali
kwa Chama cha Tanzania Peoples Part (TPP) kutoshiriki katika shughuli zozote za
kisiasa zinazoendelea nchini. Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Kauli hiyo imekuja baada ya
Chama hicho kuonekana kuendelea na shughuli za kisiasa wakati kilishafutiwa
usajili wake
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,
Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahoza amesema chama hicho
kilishafutiwa usajili tangu Machi 20, 2002, chama kikishafutiwa usajili wake
hakitakiwi kufanya shughuli zozote za kisiasa.
Nyahoza amesema ameshangazwa sana na watu waliojitokeza na
kujitambulisha kuwa ni viongozi wa chama hicho waliojitokeza katika vyombo vya
habari na kuanza kunadi sera licha ya kuwa chama hicho kilifutwa.
“Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa sura ya 358 kifungu cha
7(3) inakataza taasisi yoyote kufanya shughuli za kisiasa bila kusajiliwa na
msajili wa vyama vya siasa.
“Sheria ya vyama vya siasa kifungu cha nane(b) ambacho kinazuia
mtu yoyote kufanya shughuli za kisiasa kwa jina la chama ambacho yeye sio
mwanachama wala kiongozi,” amesema Nyahoza ambaye aliongea kwa niaba ya Msajili
wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
No comments:
Post a Comment