.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA

X2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akizungumza na watumishi mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo ina hifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
X1
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto) akizungumza na watumishi wa mashirika mbalimbali yaliyoko katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati waziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) aliyetembelea kambi hiyo jana.
X6
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile(kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu katika makazi ya wakimbizi yaliyopo Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

X7
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ,akimsikiliza mmoja wa maofisa wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) alipotembelea ndani ya mahema wanakoishi wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
X5
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kambini hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ina hifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
X4
Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Amah Assiama-Hillgartner ( kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil (katikati), aliyetembelea hospitali hiyo wakati wa ziara yake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
X3
Daktari wa Hospitali ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Florence Mshana (aliyeshika karatasi),akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mbarak Abdulwakil (kushoto), alipotembelea hospitali hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo ina hifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCH

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.