Picha na Video Kilichojiri UKAWA wakizindua kampeni Huko zanzibar

Leo ilikuwa ni zamu ya zanzibar kuzindua kampeni zao  UKAWA,mkutano mkubwa uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti pia ulihudhuriwa na mgoimbea wa Tanzania Bara Mh EDWARD LOWASA,hapa nimekuwekea Picha kadhaa na Video ya mkutano huo fwatilia kilichojiri huko
DSC_1256
DSC_1252DSC_1256 


DSC_1250
DSC_1252
Rasmi leo Chama Cha Wananchi CUF kimezindua kampeni zake za uchaguzi2015 hafla iliyofanyika uwanja wa Kibandamaiti jioni ya leo.
Viongozi kadhaa wa CUF pamoja na viongozi wa Ukawa wamehudhuria.

Mgeni rasmi akiwa ni Mgombea Urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. Pia walihudhuria Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano, Bw Edwar. Lowassa, Mgombea Mwenza wa Urais, Juma Duni Haji pamoja na wagombea kadhaa wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Viongozi wa vyama ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi CUF, Bw Twaha Taslima, Naibu Katibu Mkuu CUF,Nassor Ahmed Mazrui.
Mkutano amepambwa kwa shamrashamra huku vikundi vya sanaa, muziki, vikitumbuiza.

Katika ufunguzi wa kampeni, Mgombea Urais wa Zanzibar Maalim Seif alivishwa koja la mauwa kisha kubonyeza kitufye kuashiria ufunguzi rasmi. 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.