Kampuni ya simu ya
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Dar es Salaam Teknohama Business Incubator
(DTBi) leo wamezindua huduma inayowawezesha watumiaji wa simu za kisasa za
mkononi (smartphone) kurejesha kumbukumbu na kupatikana iwapo simu itapotea au
kuibiwa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego
Gutierrez alisema,
“Kama kampuni iliyoko
msitari wa mbele katika kuleta mabadiliko ya kidigitali nchini, huduma hii mpya
iitwayo Tigo Backup itawawezesha wateja wa Tigo kurejesha orodha ya majina
kwenye simu, picha, video, ujumbe mfupi (SMS) na vitu vingine vilivyopotea, kuibiwa
au kutokana na ubovu wa simu. Wateja wataweza pia kugundua na kurejesha simu
zao zilizopotea au kuibiwa.”
Akielezea huduma hiyo ya
kama ya kipekee, Gutierrez alisema Tigo Backup inamuwezesha mteja aliyepoteza
simu yake kuwa na uwezo wa kupata picha ya aliyemwibia kwani simu itapiga
king’ora, kuonyesha simu hiyo ilipo, simu itajifunga ili kuzuia matumizi
mabaya, kumjulisha mwenye simu pindi abadilishapo laini ya simu na pindi simu
inapopoteza habari muhimu. Huduma ya Tigo Backup imebuniwa na mwanafunzi
mzawa kutoka DTBi.
Alisema sifa zote hizi
zitawezeshwa kupitia ujumbe mfupi (SMS) au kupitia wavuti ya: https://www.tigobackup.com.”
Alisema kuwa huduma hii ya kurejesha taarifa, ‘Tigo Back up’ itamgharimu mteja
Tsh. 500/= kwa mwezi ilhali huduma nyingine kama vile kurejesha kumbukumbu ya
orodha ya majina kwenye simu, taarifa ya kubadilisha laini ya simu na huduma ya
kufunga simu iliyoibiwa zitatolewa bure. Aliongeza kwamba wateja wategemee
huduma nzuri kutoka kwa Tigo huduma kwa wateja kutokana na huduma hii mpya
itakayowawezesha kupata ulinzi mzuri dhidi ya wizi wa simu zao.
Sifa tofauti zaidi
kutokana na huduma hii ya kurejesha kumbukumbu ya usalama yaani Tigo Backup, ni
kwamba mtu hahitaji kuunganishwa na intaneti ili kupata huduma hio. Mtu anaweza
tu kufuatilia bure simu iliyopotea au kuibiwa, mahali na taarifa za mtu anayetumia
simu hiyo. Huduma hii itapatikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwaajili
ya matumizi ya Watanzania wote kwa ujumla.
Hafla ya uzinduzi huo
ilihudhuriwa na Waziri wa Mazingiri dkt.Binilith Mahenge aliyesisitiza
kuwa jitihada
zza serikali kuendelea kujenga mazingira mazuri ili kusaidia ukuaji wa tasnia
ya tehama na kuifanya iwe na mchango mkubwa kwa kipato taifa na kutoa ajira
nyingi kwa vijana.
“Lengo letu ni kuendeleza kundi kubwa la
rasilimali watu la TEHAMA, ikiwa ni pamoja na ubunifu wa programu za kwenye
kompyuta katika ngazi zote ili kuziba pengo la kidijitali (vijijini na
mijini)”, alisema Dkt.Mahenge.
Kwa upande wake
Mhandisi George Mulamula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi alisema
kuwa Tigo Backup ni matokeo ya ushiriakiano baina ya kampuni ya Tigo Tanzania
na DTBi wakiwa na lengo la kukuza na kuendeleza huduma za kidigitali kama
chachu ya maendeleo kwa jamii.
“DTBi imeendeleza kampuni ya Magilatech ambayo ni kampuni ya habari na
mawasiliano inayoendeshwa na vijana wa Tanzania.” Aliwashukuru Tigo kwa kuwa na
malengo sawa na DTBi la kuendeleza vijana na wanawake wa Tanzania katika
kuwaandalia mbinu za kupambana na kuondokana na matatizo ya kijamii kwa
kuwaandalia nafasi za kazi nchini.
Akifafanua kuhusu huduma
hiyo ya Tigo Backup kuwa na uwezo wa kurejesha kumbukumbu ya simu, “Ili kupata
huduma hii, mtu anatakiwa kuwa na laini au namba ya Tigo iliyosajiliwa na simu
ya kisasa yenye mfumo wa android, kuihifadhi kwenye simu yake kutoka kwenye
Playstore na usajili kufuata kwa kuingiza namba yake ya simu, neno siri na
anwani ya wavuti,” Huduma hii itapatikana kwa watumiaji wa simu za kisasa zenye
mfumo wa android kwanza na kisha baadaye kwa wale watumiaji wa simu zenye mfumo
wa IOS.
No comments:
Post a Comment