Wednesday, September 9, 2015


Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa vilabu 16 vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofnayika leo ofisi za TFF zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.
Tumekua na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.
Naye Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote yatakayofnayika ndani ya nchi.
Mchezaji au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiw akatika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Lengo letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa NHIF umevipunguzia vilabu mizigo wa matibabu na sasa vilabu vitaweza kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.

No comments: