Wednesday, September 9, 2015

WLAC waendelea kuwapiga msasa wanawake mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu Mwaka huu

Mwezeshaji kutoka Dodoma FORTUNATA MAKAFU akiwasilisha mada katika mafunzo hayo yanayofanyika Jijini Dar es salaam kwa wanawake malimbali lengo likiwa ni kuwajengea uelewa zaidi juu ya maswala ya uchaguzi ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.PICHA NA EXAUD MSAKA HABARI
 Kituo cha msaada wa sheria nchini Tanzania WLAC kwa udhamini wa shirika lisilo la kiserikali la OXFAM wameendelea na mkakati wao wa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali nchini Tanzania vya wanawake kuwajengea uwezo na uelewa juu ya harakati za uchahuzi mkuu unaoendelea nchini Tanzania ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huo.

Leo jijini Dar es salaam Mchakato huo uliwalenga wakina mama ambao ni viongozi wa vikundi maarufu vya VIKOBA ambao nao wamepata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo ambayo yameelezwa kuwasaidia wanawake hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Mtandao huu ulihudhuria katika mafunzo hayo na kubahatika kuzungumza na moja kati ya waratibu wa mafunzo hayo ambaye ni mwanasheria kutoka WLAC Bi FAUDHIA YASIN ambaye amesema kuwa mafunzo hayo leo yamendelea kwa kuwakutanisha wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vya VIKOBA katika wilaya ya kinondoni ambapo mchakato huo utaendelea katika wilaya nyingine na maeneo mbalimbali nchini.

Katika mijadala mbalimbali iliyokuwa inaendelea katika mafunzo hayo imeelezwa kuwa hali inaonyesha wanawake wamekuwa wakionekana kuwa nyuma sana katika maswala ya siasa hasa maswala ya kushiriki katika kampeni na kusikiliza sera za wagombea jambo ambalo limewafanya wanawake kuchagua viongozi ambao hawakusikia sera zao kwa ujumla.

Mwanasheria kutoka kitoka kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC akizngumza na wanahabari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea katika mafunzo hayo Jijini Dar es salaam
Akizungumza na mtandao huu nje ya mafunzo hayo moja kati ya wawezeshaji wa leo Bi FORTUNATA MAKAFU amesema kuwa ni kweli  wanawake wengi wamekuwa wakichaguliwa viongozi na wanaume kutokana na wao kuwa nyuma sana katika swala la kusikiliza sera jambo ambalo amesema pia linachagiwa na mfumo Dume uliotawala katika uchaguzi.

No comments: