Tuesday, September 8, 2015

ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA

Byesige Josephat (anayemiminamafuta) na HezronMtangirwa(kushoto), wakimbizikutoka Burundi waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wa kipima mafuta ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana ,baada ya kugawiwa mafuta na Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikiachakula (WFP), ambalo linakituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma 
Kinamama wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao waunga unaotolewa kwa wakimbizi wanao hifadhi wa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.  Serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka  Burundi wanapata chakula cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yao.
Mkimbizi  Irene  Ntibelenda (katikati) akiwapamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) baada ya kupokea mgao wa chakula unaotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililona Kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma .Kushoto ni mtoto wake aitwaye Nsengi yumvaI diphonce.


Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Josef Ntukugurya akifunga shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kupokea unga huo kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa, linashughulikiachakula(WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya Nyarugusuil iyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma
Sehemu ya shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafutayakupikiaikiwakatikaghala la kuhifadhia chakula lililopo katika  kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma .Chakula hiki hutolewa na Jumuiya ya Kimataifa kama kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP) ilikusaidia wakimbizi wanaohifadhiwa hapa nchini.
Wakimbizi kutoka nchini Burundi  walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments: