Sunday, October 4, 2015

ACT WAZALENDO wamlilia Marehemu MTIKILA


CHAMA cha Alliance For Change and Transparance,( ACT- Wazalendo.)kinachozingatia misingi ya utu, undugu  na uzalendo kwa Taifa,kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Christopher Mtikila, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Democratic (DP).


 Chama kinatoa salamu za pole kwa  familia ya Marehemu, ndugu jamaa na marafiki,Makamu Mwenyekiti wa DP Taifa,Mwenyekiti wa mabaraza ya Vyama vya Siasa na Watanzania kwa ujumla.
ACT wazalendo inatambua mchango wa kina wa kutafuta mageuzi ya kweli yaliyokuwa yakiendeshwa na Mchungaji Mtikila wakati wa uhai wake
Tunaami mchango wake kwa Taifa ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu katika nchi
Tunawaombea kwa mungu familia yake  wawe na uvumilivu na kuzidi kumuombea marehemu apate pumziko la amani.
ACT-Wazalendo tutazidi kumuombea kwa Mungu ampe faraja katika utangulizi wake huu, huku tukiwa na mengi mema ya kujifunza kutoka kwake.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe 
Imetolewa na
  Samson Mwigamba
Katibu Mkuu Taifa ACT-Wazalendo

04/10/2015

No comments: