Saturday, October 3, 2015

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri

ChristopherMtikila
Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa “Taarifa za mwanzo” zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Pwani
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu tutakujuza hivi punde
mtikila
Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.
Mtandao wa HABARI24 BLOG unaungana na watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba,mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi

No comments: