Thursday, October 1, 2015

ANZA KUFAIDI PICHA 100 NA ZAIDI ZA LOWASA DAR ES SALAAM LEO

MGOMBEA urais aliyeteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa ametangaza rasmi kuwa ana shida ya kura milioni 14 ili atangazwe rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lowassa ametaka wale wanaomuunga mkono kote anakopita tangu kuanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba 25, wajitokeze kwa wingi na kumthibitishia kumpenda kwa kumpigia kura nyingi.
Amesema iwapo watazipiga kwa wingi siku hiyo, wabaya wanaopanga kumuibia kura zake, hawatafanikiwa kwa sababu watajikuta wakizidiwa na kura alizopigiwa na Watanzania.
“Nipigieni sana kura zenu, nataka kura milioni 14 na ushei ili kuwa rais mpya wa serikali ijayo ya watu itakayoongozwa na watu walio makini,” amesema huku akijinasibu kuwa anagombea urais kwa sababu ana uwezo wa kuwa rais na amechoshwa na umasikini unaowaumiza Watanzania.
“Tutaongoza kwa umakini mkubwa, hatutaki fujo zozote sisi, ni chama cha watu makini. Mimi nagombea urais kwa sababu naweza kuwa rais, nimechoka kuona watu wanalalia mlo mmoja kwa siku, nimechoka, na nina hasira za kupambana na umasikini. Ndio maana nasema kipaumbele change cha kwanza cha pili na cha tatu itakuwa ni elimu ambayo ndiyo inayowatoa wananchi katika umasikini,” amesema mara baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi wasilale baada ya kupiga kura.

Mbowe amesema safari hii hakuna mtu kwenda kulala akishapiga kura. “Piga kura yako na ukishatoka nje ya kituo, hesabu hatua moja, ya pili na ukifika hatua mia moja hapo kaa ulinde kura.

“Hatutalala na hatutaacha kukesha kulinda kura zetu,” alisema na kupokewa kwa sauti kubwa ya kuungwa mkono na umma uliofika kwenye mkutano huo wa mwisho katika kampeni ya Lowassa mkoani Dar es Salaam.

Mbowe ambaye anatetea kiti cha ubunge jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, amesema UKAWA hawatakubali ujanja wa Jeshi la Polisi kutaka watu wasikae vituoni wakishapiga kura, kwa sababu hakuna atakayezilinda kura za mgombea wa Ukawa kutokana na mfumo uliopo wa ulinzi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu mstaafu awamu ya tatu, Frederick Sumaye amesema moja ya sababu kubwa zinazomfanya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kukosa sifa ya kuchaguliwa, ni kukurupuka katika maamuzi.
Akizungumza katika viwanja vya Tanganyika Packers, jimboni Kawe, Sumaye amesema zipo rekodi nyingi za Magufuli zinazothibitisha kuwa amekuwa mkurupukaji na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa taifa.

“Hata mwenyewe amekata tamaa, ameanza kutetea safari za nje za Mheshimiwa Kikwete, hivi rais anawezaje kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya nusu ya muda wake aliokaa madarakani? Haiwezekani hizo safari zote zikawa na manufaa kwa Watanzania, kwa kutetea kwake safari hizi, kuna hatari na yeye akafuata mkumbo huohuo,” amesema Sumaye.

“Nchi hii Lowassa akiingia madarakani zaidi ya Sh. bilioni 900 zinatakiwa zilipwe kama faini kwa kuchelewesha kuwalipa wakandarasi, hasara hii imesababishwa na Wizara ya Magufuli na kuna hasara kuhusu meli aliyoikamata ambayo serikali imeshindwa kesi na kudaiwa fidia ya Sh. Bilioni 3.2, amenunua meli mbovu na chakavu akidhani ni mpya, leo hii kwa aibu ile meli haifanyi kazi tena Dar,” amesema.

“Ni mtu huyuhuyu ambaye alitaka kubomoa mpaka jengo la TANESCO wakamuwahi na kumshika shati, yeye hajui kama hilo jengo ni mabilioni ya walipa kodi yametumika kujenga, anajua kubomoa tu matokeo yake mpaka wanamshika shati alishabomoa jengo la serikali la TANROAD na katika kuthibitisha kuwa zilikuwa pupa jengo hilo limeanza kujengwa upya palepale lilipovunjwa,” amesema kabla ya kuongeza:
“Magufuli ni mtu wa maamuzi ya pupa sana. Katika nchi zinazofuata utawala bora alitakiwa kulipa hizo gharama… sasa huyu anataka urais, tumeona akiwa waziri tu anakurupuka na watu wanawahi kumshika shati, hivi akiwa Rais nani atamshika Rais shati?”

Ziara ya kampeni ya Lowassa akifuatana na Sumaye, kesho inatarajiwa kuingia mkoani Manyara, nyumbani kwao Sumaye ambaye alikuwa mbunge wa Hanang’ kwa miaka kumi akiwa waziri mkuu.





































































TWENDE SINZA SASA
 
 

 
 
 
 




















 BARABARANI ALILAKIWA NA WATU KILA APITAPO
 








Sehemu ya wananchi wakiwa wamependa juu ya jengo la Tanganyika Packers ili kumshuhudia Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa alipohutubia katika viwanja hivyo
PICHA KUTOKA FURAHIAMAISHA BLOG

  

No comments: