Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida wakati akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Dk. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali hasa za mashirika ya dini ambazo zinaendesha hospitali katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma za kiafya kwa jamii.
Dk. John Pombe Magufuli leo amefanya mikutano katika miji ya Bahi, Manyoni, Itigi na Ikungi huku akifanya mingine isiyo rasmi katika maeneo mbalimbali akiwa jiani kutoka mkoani Dodoma kuelekea Singida ambako kesho ataendelea na kampeni zake kabla ya kuanza mkoa wa Manyara. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE IKUNGI -SINGIDA)
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Jonathan Njau wakiwapungia wananchi mikono kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi leo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi.
Mmoja wa wasanii walikokuwa wakitumbiuza katika mkutano huo akiwa ameshikilia bango lenye picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Ndugu Jonathan Njau katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mnadani Ikungi leo.
Baadhi ya akina mama wakiwa wamekaa kandokando ya mkutano huo huku mmojawapo akiwa ameshilikilia picha ya Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea huyo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshikilia vipeperushi vyenye ujumbe wa kampeni za mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli huku wakimsikiliza wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Magharibi Lazaro Nyalandu akipmigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani ambapo amewaambia wananchi wa jimbo hili kujifikiria mara bili na kuchagua mbunge kupitia CCM ili waweze kusonga mbele kwa maendeleo kutokana na kudorora kwa muda mrefu kwa sababu ya kukwamishwa na mbunge kupitia upinzani aliyeshindwa kuwaletea maendeleo kwa muda wote wa miaka mitano.
Kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka mkoani Tabora aliyejiunga na CCM hivi karibuni akitokea Chadema Mtemi Nyanda akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
Kundi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.
Chege na Temba kutoka TMK Family wakitumbuiza katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Msanii Msami pamoja na kundi lake wakitumuiza katika mkutano huo uliofanyika Ikungi kwenye uwanja wa Mnadani mkoani Singida.
Baadhi ya wana CCM wakifurahia jambo wakati Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia .
Burudani zikiendelea.
Msafara wa Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliukiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi Mh. Lazaro Nyalandu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Manyoni.
Baadhi ya wananchi wakiwa na shamrashamra wakati wakimpokea Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani alipowasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Manyoni mkoani Singida
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni Daniel Mtuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni kushoto ni Kapteni John Chiligati aliyestaafu na kumwachia kijiti mgombea huyo.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni Daniel Mtuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akisalimiana na Mh. Lazaro Nyalandu mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Bahi.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa kulia na mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel katika mkutano wa kampeni uliofanyika Babati
No comments:
Post a Comment