Friday, October 2, 2015

Mkutano wa Kampeni Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein Gando Wete Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg Vuai Ali Vuai, wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Gando Wete Pemba kuhudhuria mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Gando alipowasili katika viwanja vya mpira gando Wilaya ya Wete Pemba kuendelea na mikutano yake ya Kampeni Kisiwani Pemba.
 Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya mkutano Jimbo la Gando Wilaya ya Wete Pemba.
   Kada wa CCM Balozi Amina Salum Ali kulia akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Maua Daftari wakiwa katika viwanja vya Gando wakihudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.  
 Wanachama wa CCM Jimbo la Gando Pemba wakifuatilia Mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba.
 Mgombea Urais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, akibadilisha mawazo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg. Hamad Mberwa Hamad. Dk Shein akiwa katika ziara yake ya mikutano ya kampeni ya kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua kwa mara ya pili kuiongoza Zanzibar.  
 Wasanii wa Kikundi cha Profesa Gogo wakitowa burudani kwa Wananchi katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Wete Pemba.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg. Hamad Mberwa Hamad, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM,na kutowa shukrani za Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kazi nzuri iliofanywa na Dk Shein, katika kipindi chake cha miaka mitano inayomalizika na kuwata Wananchi kumpa kura za Ndio ili kuiletea maendeleo Zanzibar. 
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Bi Modline Castico akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Gando kisiwani Pemba wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Pandu Ameir Kificho akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba Jimbo la Gando wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
 Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Gando.
Mgombea Urais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Gando wakati wa ziara yake ya kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, akitangaza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.katika mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya mpira Gando Pemba.   
Wanachama wa CCM wakifuatilia hutuba ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,akiwa katika mikutano yake ya Kampeni Kisiwani Pemba.
 Wananchi wakiwa makini wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. akiwahutubia na kuelezea Sera za CCM kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM.ikiwa na mikakati ya kuboresha hali za Wananchi wa Zanzibar na kuimarisha Uchumi katika sekta mbalimbali. 

Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakati akihutubia umati wa Wananchi wa Wilaya ya Gando Jimbo la Gando Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Gando akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa Kampeni Kisiwani Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 



No comments: