Wagombea wa nafasi za
udiwani na ubunge ambao ni wanawake katika uchaguzi mkuu wameomba vyombo vya
habari pamoja na wadau wa uchaguzi nchini kuwapa kipaumbele katika nyakati hizi
za kampeni kutokana na kile walichodai kusahaulika na kipaumbele kikubwa kupewa
wagombea wanaume katika uchaguzi wa mwaka huu.
Wagombea mbalimbali walioshiriki katika mafunzo hayo wakichangia mada katika mafunzo hayo |
Wito huu umetolewa leo
jijini Dar es salaam wakati wa mafunzo kwa wagombea wa nafasi hizo wanawake
nchini Tanzania mafunzo ambayo yameandaliwa na kituo cha sheria na haki za
binadamu nchini LHRC kwa udhamini wa shirika la kimataifa la wanawake la
UN-WOMEN,mafunzo ambayo yamefanyika kwa siku mbili Jijini Dra es salaam.
Wakizungumza na
wanahabari wakati wakitoa tamko lao juu ya mwenendo wa uchaguzi huo mgombea
ubunge wa jimbo la ubungo kwa tiketi ya ACT-wazalendo Mama NYANJURA NYARINDO
pamoja na mgombea ubunge wa ubungo kwa tiketi ya chama cha TLP Mama GODLIVA
MANUMBA wamesema kuwa katika hatua hii ya kampeni wanawake wamekuwa wakiwekwa
nyuma sana na vyombo vya habari pamoja na wadau wa uchaguzi jambo ambalo
wamesema linazidi kuwarudisha nyumba katika harakati zao za uchaguzi huo.
Aidha wamesema kuwa
changamoto nyingine ambayo inawarudisha nyuma wagombea wanawake katika uchaguzi
wa mwaka huu ni changamoto ya rasilimali ambayo imekuwa ikiwafanya kushindwa
kuendesha shughuli zao za kampeni huku wakiwaomba wadau kuhakikisha
wanawasaidia ili waweze kufanikisha ndoto zao katika uchaguzi huu.
Nao waandaaji wa
Mafunzo hayo ambayo ni LHRC kupitia Afisa Program wa dawati la jinsia na watoto
NAEMY SILAYO amesema kuwa lengo kuu la kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo
wagombea wanawake wa udiwani na ubunge katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania
ili waweze kupambana na kasi ya uchaguzi iliyopo sasa nchini.
Afisa Program wa dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC ,NAEMY SILAYO akizngumza na wanahabari juu ya mafunzo hayo na malengo yao kwa wagombea hao. |
Amesema moja kati ya
malengo ya mafunzo hayo pia ni kuhakikisha kuwa wanawatoa wanawake hao katika
fikra za kuamini kuwa wanaweke hawawezi na kuwarudisha katika fikra za kuamini
kuwa wanawake wanaweza kama wakiwa na nia na kujituma pamoja na kuwapa mbinu
mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia katika uchaguzi huo ili waweze kushinda
nafasi ambazo wanawania.
Aidha NAEMY amevitaka
vyama vya siasa kuhakikisha kuwa vinatoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume
katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ambapo kwa sasa amekiri kuwa nafasi
ya wanawake ndani ya vyama vya siasa bado ni finyu.
No comments:
Post a Comment