Tuesday, October 13, 2015

Tizama Alichokifanya mama Regina Lowasa Huko Iringa jioni hii

Mke wa mgombea urais kupitia UKAWA, Mama Regina Lowassa leo amefanya mkutano mkubwa mjini Iringa na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo. Mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) kwa lengo la kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Peter Msigwa na Madiwani wanaotokana na umoja wa Ukawa pamoja na Rais.
Mama Regina alisema ''Naomba nichukue nafasi hii kumuombea kura mgombea urais Mh. Edward Ngoyai Lowassa ambae ni Mume wangu, namuombea kura zote bila kuwasahau Madiwani na Mbunge''

Mama Regina amewakumbusha wananchi kuwahi mapema kwenye vituo vya kupigia kura, kuzingatia sheria za uchaguzi na namna ya kukunja karatasi baada ya kupiga kura na wasisahau kwenda na karamu zao.













No comments: