Friday, October 9, 2015

Mauzo katia soko la hisa yamepanda kutoka bilioni 2 hadi bilioni 12 katika kipindi cha wiki moja.


 



Hayo yamesemwa na afisa anayeshughulikia masuala ya biashara kutoka soko la hisa Bw Patrick mususa mapema wiki hii wakati alipokuwa anazungumza na wandishi wa habari.

Mususa amebainisha kuwa ukuaji wa mtaji wa makampuni ya ndani ndo uliopelekea mauzo hayo kupanda hadi kufikia zaidi ya pesa za kitanzania bilioni 12.

Aidha Bw mususa ameyataja makampuni ambayo hisa zake zimeuzwa sana kuwa ni pamoja na banki ya crdb kwa asilimia 77%,kampuni ya pili ambayo ambayo hisa zake zimeuzwa ni twiga cement kwa asilimia 21% ya mwisho ni kiwanda cha sigara cha tcc kwa asilimia 3.8.Hata hivyo mususa  amebainisha kuwa watu wanaweza kununua hisa kupitia menu ya cm ambayo ni*150*36#

No comments: