Monday, October 5, 2015

Mgombea Urais wa CCM, Dkt JOHN MAGUFULI azibomoa Ngome za CHADEMA kanda ya Kaskazini

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipokuwa akiondoka uwanjani baada ya mkutano wa kampeni kumalizika mjini Karatu, mkoani Arusha.

Akihutubia katika kutano huo, Dk Magufuli aliwaambia wananchi wa Karatu kuwa mmoj wa viongozi wa upinzani anaowapenda kwa dhati ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa kwani ana misimamo thabiti na ana mapenzi makubwa na nchi yetu.
 

 Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Karatu, Arusha.

Wananchi wakishangilia kwa kunyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura za ndiyo mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli mjini Karatu.
 

 Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara.

 Moja ya mabango ya kumsifia Dk Magufuli yaliyokuwepo katika mkutano wa kampeni mjini Karatu.

 Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwaonesha wananchi kwenye mfano wa  karatasi la kupigia kura, picha ya kwake na ya  Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan ambayo ipo nafasi ya tatu, wakati wa mkutano wa kampeni mjini Katesh, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.
 

 Wananchi wa Kateshi wilayani Hanang wakishangilia Dk Magufuli alipowasili kwenye uwanja wa CCM katika mkutano wa kampeni mjini Katesh.

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Katesh, wilayani Hanang.

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Hanang, Dk Mary Nagu mjini Katesh, Hanang leo.

 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli na kukubali kumpigia kura ili ashinde urais.

 Baadhi wananchi wakiwa juu ya miti ili wape kumuona Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Katesh.

 Moja ya mabango ya kumsifia Dk Magufuli yaliyokuwepo katika mkutao wa kampeni katika Mji wa Hydom, wilayani Mbulu.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za Dk Magufuli, Alhaji Abdallah Bulembo akielezea wasifu wa Dk Magufuli  kuwa anafaa kuwa rais wa Tanzania badala ya Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa.

 Wakazi wa Hydom wakiwashangilia hotuba ya Dk Magufuli huku wakiwa juu ya mti.

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Hydom, wilayani Mbulu, Manyara ambapo aliwataka wananchi kutowachagua wagombea wanaotoa rushwa kwani wakikubali wanaweza wakawauza wao na Tanzania kwa ujumla.

 Wananchi wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli kuwa Rais wa Tanzania, wakati wa mkutano wa kiampeni mjini Hydom, Mbulu.

 Ni furaha tele kwa wakazi wa Hydom baada ya kumuona Dk Magufuri.


 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Masay mjini Hydom leo.

 Dk Magufuli akicheza ngoma ya kabila la Wambulu, wialani Mbulu.

 Dk Magufuli akihutubia na kuwaomba kura wananchi katika Tarafa ya Dongobash, wilayani Mbulu leo.

 Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya miti ili wapate kumuona vizuri Dk . Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Tarafa ya Dongobesh, wilayani Mbulu.

 Wananchi wakiwa na mfano wa jembe na nyundo alama zinatumiwa na CCM zenye maana ya chama cha wakulima na wafanyakazi. Vifaa hivyo walimuonesha Dk Magufuli katika Kijiji cha Bashel, wilayani Mbulu, huku wakimwimbia wimbo.

 DEk Mary Nagu  akimuombea kura mgombea urais wa Tanzania, Dk Magufuli mjini Mbulu.

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Mbulu.


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa  mkutano wa kampeni  mjini Karatu, mkoani Arusha.

 Wananchi wakimpungia mikono Dk Magufuli ikiwa ni ishara ya kumuaga baada ya mkutano wa kampeni kumalizika mjini Karatu.

Dk Magufuli akiwaambia wananchi wa Karatu kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda kwa dhati ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa kwani ana misimamo thabiti na mapenzi makubwa na nchi yake Tanzania.

No comments: