Kampuni
ya mafuta na gesi ya Swala Tanzania plc inapenda kutaarifu kwamba
imechagua eneo kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha mafuta na utafutaji
kwa mwaka 2016 ambao utafanyika kwenye
eneo tarajiwa la Kito kwenye leseni ya
Kilosa- Kilombero.
Akifafanua
kuhusu kuanza kwa uchimbaji huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swala, David Mestres
Ridge alisema kuwa tafsiri ya marudio ya 2013 na 2014 ya takwimu za mirindimo
zimesababisha kuboreshwa kwa uelewa wa
eneo tarajiwa la Kito, huku akiongeza
kuwa tathmini za mirindimo zilizopo zimebainisha kuwepo umbo la ziada kwenye
ufa unaopakana na bonde hilo la Kito
lilopo upande wa magharibi mwa bonde la Kilombero.
“Tafsiri mpya za takwimu kwenye bonde la Kito
zimeonesha kuongezeka kidogo kwa ukubwa muundo wa ramani iliyotengenezwa
awali wakati mapitio ya awali ya muundo huo wa ziada yameiwezesha kampuni kukubaliana na hazina iliyopo kwenye bonde la Kilombero.
Ridge alisema, “Mapitio ya kiufundi kwa Bonde
la Kilombero yanaonesha matarajio ya Kito
yatakuwa makubwa na yametoa
vidokezo vya matumaini vya kuwepo rasilimali muhimu ndani ya bonde hilo.
Kampuni ya Swala ipo kwenye mchakato wa kumalizia tathmini ya athari za mazingira (EIA) kwenye
maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya uchimbaji na pia kutafuta wakandarasi wa
uchimbaji kwa ajili ya kisima cha utafutaji mafuta cha Kito kwa mwaka 2016.
Kuhusu
Swala:
Swala ni kampuni iliyo chini ya kivuli cha Swala Energy
Limited, kampuni ambayo kwa upande wake iko kwenye orodha ya soko la hisa la
nchini Australia (ASX) na ikijulikana kwa kifupi kama "SWE". Swala
inamiliki mali katika nchi za Afrika Mashariki zinazopitiwa na mfumo wa bonde
la ufa na ina ardhi yenye eneo la zaidi ya kilomita za mraba 17,500. Swala
inafanya kazi kwa juhudi na ina mpango wa maendeleo ya biashara ili kuendelea
kukua hasa katika majimbo ya Afrika Mashariki yenye nishati ya hydrocarbon.
No comments:
Post a Comment