Thursday, October 8, 2015

PICHAZZ--Lowasa huko arusha ni balaaa,Tizama ya huko leo

Edward Ngoyai Lowassa na Godbless Lema wakiwasili katika viwanja vya Sinoni Unga Ltd leo Alhamisi 8/10/2015

Sumaye:

Sina tatizo na Magufuli, lakini siyo kwa nafasi ya rais, Magufuli mwenyewe hana imani na chama chake ndiyo maana anasema chagua magufuli.

Magufuli anasema ccm ni sawa na kitanda chenye kunguni. Anamkaribisha Lowassa jukwaani Lowassa:

Naomba kura nyingi ili niweze kushinda.
Nimeomba kuwa rais kwasababu nimechoka na umaskini.
Nitaanza na elimu ili kuondoa hali ya umaskini. Vipaumbele vyangu vya kwanza elimu pili elimu tatu elimu. Ukimpa mtoto wako elimu umemsaidia kimaisha. Nimesema elimu kuanzia nursery hadi chuo kikuu bure. Wanasema haiwezekani mimi nasema inawezekana kabisa tuna fedha nyingi sana nchi hii kuanzia gesi mpaka madini na utalii. Hakuna mwanafunzi kulipa mchango wa aina yoyote. Nitazingatia maslahi ya mwalimu ili awe na moyo na kazi yake.


Eneo la pili ni eneo la kilimo nitaiboresha na mkulima akitaka kuuza mazao yake popote auze. Tuwape wananchi uhuru wafurahie matunda ya nchi yao wakale raha
Eneo la tatu ndugu zangu wa bodaboda, mama ntilie na machinga watakuwa rafiki wa serikali yangu. 

Naahidi nikiingia ikulu baada ya wiki moja atakayewasumbua nakula nao sahani moa. Nitaanzisha benki kwa ajili wa wamama kupata mikopo.
Nikichaguliwa kuwa rais kila wilaya kutakuwa na hospitali za rufaa zenye vifaa vya kisasa kuwasaidia wagonjwa.
Nimekusudia kuongoza Tanzania kwakuwa nia ninayo sababu ninayo na uwezo ninao. Serikali yangu itakuwa ya mchakamchaka

Sumaye:
Hatuhitaji rais mbabe, Magufuli ni rafiki yangu lakini hafai na haiwezekani awe rais
Sumaye:
Tumepitia maeneo mengi ya nchi, mazingira tunayoyaona kila mahali inafanana na hapa Arusha, hivyo watanzania wamedhamiria mabadiliko.

CCM waliahidi ahadi nyingi, bado watu wanakosa huduma za afya, kikwete aliahidi kuwa akiingia madarakani kuwa tatizo la ajira kwa vijana itakuwa historia sasa nawauliza amelitatua? Watu hapanaaaa.... Kinana juzi ametuambia rushwa imekuwa tatizo ccm, hata juzi amewaambia hapa Arusha, sasa kama wameona hili wanasababu gani ya kutuomba kura zetu, kwanini wanashindwa kutuambia wakae pembeni?

Magufuli wizara yake inaongoza kwa rushwa na ufisadi.. Wizara yake imesababisha zaidi ya bil 125 serikali inadaiwa na wakandarasi kwa uzembe wa wizara yake, zaidi ya bilioni 900 ni malipo hewa uadilifu wa Magufuli uko wapi?
Rais ni mtumishi wa umma, waanchi ndiyo boss wa rais, magufuli hiyo sifa hana ndiyo maana aliwaambia wannachi wasioweza kulipa nauli ya feri wapige mbizi. Kule chato Magufuli aliwaambia wananchi kama wanataka lami wakajisaidie barabarani iwe lami




KADA Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi CCM,Kingunge Ngombale –Mwiru ambaye amekiaga chama hicho ,ameendelea kukitolewa lawama cha hicho kusema CCM pumzi yake imefikia mwisho na hakitakiwi kupewa tena dhamana ya kuongoza nchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

     Akizungumza  wakati wa Kampeni za kumnadi Mgombea Urais kupia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vya Ukawa,Edward lowassa zilizofanyika leo Arusha Mjini na kushuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao uliosababisha shughuli nyingi kusimama.
       Ambapo Kingunge  amedai chama chake hicho kilichomlea kimechoka na hakina nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania anayeishi kwenye lindi kubwa la umasikini.
      Amesema CCM anayoijua yeye tangu ilipokuwa TANU ilikuwa yenye misingi na kuweka mipango ya kumletea maendeleo moja kwa moja Mtanznaia, lakini amedai CCM hile sio hii ya sasa kwani hii ya sahivi imetekwa na watu wachache wenye kujali maslahi binafsi na sio kumleta maendeleo mtanzania.
       Kingunge huku akishangiliwa kwa nguvu,amemshukia pia Rais Jakaya Kikwete kwa kusema utawala wake umeua uchumi wanchi,
“Leo uchumi wa nchi umeporomoka,wakati Mkapa anamwachia nchi Kikwete uchumi ulikuwa kwenye hali nzuri,lakini baada ya kuingia yeye uchumi wan chi umedorola huku umasikini unazidi kuwa mkubwa kwa watanzania’
  SUMAYE ANENA.
Kwa upande wake Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu,Fredrick Sumaye amewataka watanzania kutomchagua Mgombea wa Urais kupitia CCM John Magufuli kwani mgombea   huyo anamaamuzi ya kukurupuka na ambaye tena asiyekubali kushaulika jambo ambapo  amewasihii Watanzania wakimchagua kuwa watakuja juta.
     Sumaye ambaye ni waziri mkuu peke aliyeongoza kipindi kilefu amesema hata  wizara alizopewa  Magufuli kuongoza ameonyesha utendaji wa kibabe usiofuata utu na uzalendo kwa watanzania.
  LOWASSA ANADI SERA.
Kwa upande wake Mgombea wa Urais kupiatia mwavuli wa Ukawa Edward Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anapambana katika kuondoa umasikini kwa watanzania.
“Ninagombania nafasi ya Urais kutokana na kuchoka kusikia habari ya Umasikini,nimedhamilia kupambana na umasikini,nimechoka kusikia watu wanakula mlo mmoja,nataka nikiingia tuwe tunajadili milo mitatu,ambaye ana ngombe mmoja awe na Ngombe wa wili”amesema lowassa.
Lowassa pia ameendelea kushikilia ilani yake ya elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu huku akiwapinga wanaibeza ahadi yake hiyo kwa kusema nchi hii inapesa nyingi zinazopotea kwenye Mgari ya kifahali.
  KUHUSU TANESCO.
Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha analifufua shirika la Umeme nchini TANESCO ndio litakuwa jambo lake la kwanza na kulifanya shirika hilo liondokane na mgao wa umeme.
  LEMA AFUNGUKA.
Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjinia kupitia Chadema Goodbress Lema ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC kupeleka haraka karatasi za kupigia kura kwenye mkoa wa arusha ili wananchi wawajue wagombea wao.
Amesema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo la Arusha wamezamilia kwa kauli moja kumchagua Lowassa.













No comments: