Friday, October 16, 2015

RAIS TFF ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.

No comments: