Monday, October 26, 2015

Sentensi 11 kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi TACCEO mchana huu

Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia changzi nchini Tanzania TACCEO ambao wanaratibiwa na kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini LHRC umeendelea kutoa tathmini ya maswala kadhaa wanayoyaona katika zoezi nzima la kupiga na kuhesabu kura.Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA mchana huu akizngumza na wanahabari.Hapa nimekuwekea sentensi kadhaa walizotoa leo hii kuhusu zoezi hilo
1-Maeneo kadhaa ya nchi ya Tanzania  hata baada ya zoezi la kupiga  kura waliendelea kupiga kura hata baada ya muda kumalizika lakini wengi walimaliza kwa muda husika

2-Swala la kuhesabu kura—90% kura ziolihesabiwa vituoni lakini asilimia moja hazikuhesabiwa vituoni

3-Swala lingine ambalo limerepotiwa na mawakala wetu walioko nchi nzima ni kuwa 99% ya mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu waliruhusiwa kuwepo kwa mujibu wa sheria wakati wa kuhesabu kura.

4-Pia 99% wa ccm na Chadema walikubaliana na matokeo na kutia saini katika nakala za matokeo.

5-Wakati wa zoezi la uhesabuji kura vijana waliokuwa wanasubiri matokeo katika mitaa mbalimbali ya nchi walikabiliana na polisi na mabomu tukio ambalo pia leo limejitokeza katika maeneo ya Temeke ambapo baada ya wasimamizi kuchelewesha matokeo kubandika wananchi walikusanyika na kutaka kupewa matokeo yao jambo ambali lililazimu polisi kuwatawanya kwa mabomu.

6-Mchana wa leo pia huko Zanzibar mabomu yamepigwa kutokana na sakata ambalo limeibuka leo ambapo mgombea wa chama cha wananchi CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD alitangaza kuwa ameshinda uchaguzi huo kutokana na matokeo ambayo ameletewa na mawakala wa chama chake hivyo watu kulipuka na furaha hali ambayo imezua tafrani huko Zanzibar.

7-Nia rai yetu kuwa zoezi la uhesabuji wa kura likafanyika kwa umakini mkubwa na ili kuepusha fujo na hiyo inasababisha watu kukosa uvumilivu na kujitangazia matokeo wenyewe na kusababisha rapsha mitaani

8-Tunaomba hali ya utulivu na amani lakini tukumbuke kuwa haki ndio tunda la amani na kuelewana.

9-Swala la kujumlisha matokeo sio baya ila kujitangazia matokeo ni mbaya sana kwa sababu wanakuwa wanachochea uvunjifu wa amani.

10-Tuhuma mbalimbali za kukamatwa kwa mabox zinazoenea katika maeneo mbalimbali zinasemwa lakini hakuna ushahidi wa kujitosheleza sana kumtia mtu hatiani kwa sababu tume wamekanusha na kusema kuwa hao watu ni wafanyakazi wa kawaida wa serikali na tume hivyo ni kutokuelewa tu mfano lile tukio la vunjo halijapata udhibitisho.

11-Tatizo ni kwamba wafanyakazi wa tume wanapewa vifaa vya uchaguzi lakini hawapewi usafiri wa kubebea hivyo wanalazimika kubeba na kulala navyo nyumbani hivyo ni hatari sana kwa wafanyakazi hao.

No comments: