Sunday, October 4, 2015

Tizama Lowasa Alivyotikisa manyara leo

Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edward Lowassa amesema kama atachaguliwa atahakikisha anafuta kodi ambazo zimekuwa mzigo kwa wananchi wa kipato cha chini.
Wakati upepo wa kisiasa ukizidi kubadilika na huku kadi namba 8 ya CCM ikiwa tayari imekwisha kurejeshwa Dar es Salaam, Mgombea wa urais wa Edward Lowassa anasema kama watanzania watampatia ridhaa ya kuwa rais wa nchi atahakikisha kila mtanzania ananufaika na keki ya taifa akianzia na wafanaykazi wa kada ya chini.
Uwepo wa kodi mizigo kwa watanzania wanyonge ni tatizo ambalo serikali yake italishughulikia ndani ya siku 100 za kwanza ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za jamii hasa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Akihutubia maelf ya wakazi mjini hanang ambapo amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 20, Fredrick Sumaye amewataka wanahanang na watanzania kwa ujumla kutokuhadaika na ahadi butu za CCM, kwani uongozi huo wa CCM ndio umechochea umasikini uliokithiri kwa watanzania.
Huku akitumia usafiri wa chopa amefanikiwa kuhutubia mikutano katika maeneo ya Dogobeshi, Magugu, kabla ya kuhitimisha kwa kuhutubia maelf ya wakazi wa jimbo la Hanang mkoan Manyara 











No comments: