Wakati jana Tume ya Taifa
ya uchaguzi nchini Tanzania ikitangaza kuwa sio lazima kwa wanananchi kubaki maeneo ya vituo
vya kupiga kura kwa kisingizio cha kulinda kura,nao umoja wa katiba ya wananchi
ukawa wameibuka na kuwataka wananchi na wafuasi wao kupuuza kauli hiyo na
kuhakikisha kuwa wanasimama umbali uliowekwa kisheria wa mita mia moja ili
kuzuia aina yoyote ya hujuma zinazoweza kufanywa na wapinzani wao.EXAUD MSAKA HABARI anasimulia--------
Akitangaza msimamo huo
leo Jijini Dar es salaam katibu mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo
CHADEMA JOHN MNYIKA amesema kuwa kauli ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuwa
wapinzani hao wana ajenda yao ya siri mwenyekiti huyo aleleze wazi ajenda hiyo anayosema
lakini lengo lao ni kuwapa wapiga kura
haki ya kusimamia kura zao na kuhakikisha kuwa hakuna aina yoyote ya
uchakachuaji unaoweza kufanyika.
Mnyika amesema kuwa kwa
mujibu wa sheria ya uchaguzi wapiga kura wanatakiwa kukaa umbali wa mita mia
moja kutoka kituo cha kupigia kura wakifwatilia kwa ukaribu kura zao
zikihesabika na ndicho wanachowaelekeza wapiga kura wao na hakuna sheria
itakayovunjwa hivyo akawataka wapiga kura na wafuasi wao ambao wanahitaji
kulinda kura zao kuhakikisha kuwa
wanakaa umbali huo ili kufwata sheria zilizowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
“Ni kweli kuwa tuna
mawakala wetu ambao watakuwa wanasimamia kura ndani,na tuna waamini sana lakini
tunachokisema sisi wananchi ni mawakala wengine ambao wanaweza pia
kutusaidia,tuna uzoefu wa chaguzi nyingi,maeneo mengine mawakala wetu wamekuwa
wakiichezewa rafu nyingi bila wao kujua na kujikuta washafungwa goli la
mkono,ila tunaamini wananchi wakiwa maeneo ya karibu kufwatilia kila
kinachoendelea hakuna mtu anayeweza kumchezea rafu wakala wetu wa ndani”Amesema
mnyika.
Ameongeza kuwa kufwatilia
matokeo kwa ukaribu ni haki ya mpiga kura yoyote Tanzania kwa mujibu wa sheria na
hakuna vurugu wala uvunjaji wowote wa sheria ambao unawea kutokea kama tume
ilivyoeleza hapo awali.
Aidha katika hatua
nyingine JOHN MNYIKA mbaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la kibamba ameitaka
tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha kuwa inagawa nakala ya daftari la kudumu
la wapiga kura kwa vyama vya siasa mapema ili walikague na kujiridhisha kwani
kuendelea kulichelewesha ni kuendelea kuleta sintofahamu na kufanya wananchi waamini
kuwa kuna aina ya uchakachuaji unaofanywa na tume hiyo.
“Tunaitaka tume igawe
daftari kwa vyama vya siasa haraka iwezekanavyo na sio kusema tutawapa halafu
hawatoi,kuna uwezekano mkubwa wanachelewesha maksudi ili waje walitoe mwishoni
ambapo wanajua kabisa likiwa na makosa hakutakuwa na muda wa kuhoji tena kwani
siku ya uchaguzi itakuwa imefika”amesema MNYIKA.
KUHUSU KUKAGUA MFUMO WA
UHESABUJI KURA
Baada ya jana tume chaguzi
kutangaza rasmi kuwa wataalamu wa tahema kutoka vyama vyote wataruhusiwa kwenda
kukagua mfumo utakaotumika kuhesabia kura,Mnyika amesema kuwa kusema hivyo
haitoshi na badala yake waruhusiwe mara moja kwenda kukagua na kuangalia kama
una mapungufu na sio kuja kupewa nafasi hiyo dakika za mwisho jambo ambalo
halitakuwa na faida kwani hawatakuwa na muda wa kutosha kufanya marekebisho
katika mfumo huo.
KUHUSU WANAHABARI
Wakati tume ya taifa
ikitangaza kuwa wakati wa uchaguzi mkuu waandishi wa habari watakaoruhusiwa
kushiriki kutoa taarifa za uchaguzi huo ni wale waandishi wenye press card walizopewa
na idara ya habari maelezo pekee,Mnyika amesema kauli hiyo inaweza kuzuia
upatikanaji wa taarifa hasa zile za vijijini kwani wanahabari wengi kwa sasa
hawana hizo Card na wanafanya kazi,hivyo ni lazima tume iliangalie kwa jicho la
pili swala hilo.
No comments:
Post a Comment