Mtandao wa Asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO leo umeeleza kushtushwa
kwake na mabadiliko yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani
ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC huku wakisema kuwa mabadiliko hayo hayana
ishara nzuri kwa watanzania hususani kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam Kaimu mwenyekiti wa TACCEO wakili
IMELDA LULU URIO amesema kuwa mabadiliko yanayofanywa kwa sasa ni makubwa
sana kufanyika katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kwa chombo chenye
dhamana ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi na kuhakikisha ushiriki wa
wananchi katika kupiga kura.
Amesema kuwa kwa siku
ya hivi karibuni imeshughudiwa mabadikilo makubwa ya baadhi ya watendaji na
makamishna wa tume hiyo huku akitolea mfano mabadiliko yaliyofanyika tarehe 25
mwezi wa 7 mwaka huu ambapo rais KIKWETE alifanya mabadiliko kwa kumuondoa
aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya siku ya
kupiga kura,huku pia Mkurugenzi wa technologia ya habari na mawasiliano TEHAMA
wa tume ya uchaguzi DK SISTI CARIAH akiondolewa kwenye nafasi hiyo kukiwa
kumesalia mwezi mmoja kupiga kura.
Mabadiliko mengine
ambayo TACEO wameonyesha kuwa na wasiwasi ni kuteuliwa kwa makamishna wawili wa
tume hiyo zikiwa zimebaki siku 39 kabla ya siku ya kupiga kura ambapo
walioteuliwa kushika nafasi hiyo ni pamoja na Jaji mstaafu wa mahakama kuu ya Tanzania,MARY
LONGWAY na wakili ASINA A,OMARY
Wakili IMELDA amesema
kuwa mtandao huo unaitaka serikali kuhakikisha kuwa hawafanyi mabadiliko ya
tume ya uchaguzi kwa kuwaondoa watendaji wake kwani kufanya hivyo kunaweza
kusababisha mapungufu ya kiutendaji ndani ya tume na kupelekea wananchi kukosa
imani na tume hiyo.
Aidha katika hatua
nyingine mtandao huo wa TACCEO umeitaka tume ya taifa ya uchaguzi NEC
kuhakikisha kuwa inatangaza na kuweka wazi orodha ya vituo vya kupigia kura
mapema ikiwa ni pamoja na kuweka daftari la wapiga kura siku 14 kabla ya
uchaguzi ili wananchi waweze kuhakiki majina yao na kufahamu vituo
wanavyostahili kutumia kupiga kura.
Mtandao wa kuangalia
chaguzi nchini Tanzania TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za
binadamu LHRC umekuwa ukishiriki katika uangalizi wa mchakato wa uchaguzi
nchini kuanzia zoezi la uandikishwaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa
kielektonic BVR, mchakato wa kuwapata wagombea ndani ya vyama,kampeni za
Urais,wabunge na madiwani kuelekea mchakati mzima wa uchaguzi wa tarehe 25
october mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment