MTUHUMIWA ALIYEANDIKA NA KUSAMBAZA TAARIFA ZA
UVUMI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII JUU YA KULISHWA SUMU KWA MKUU WA MAJESHI YA
ULINZI NA USALAMA GEN. DAVIS MWAMUNYANGE AKAMATWA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
linamshikilia kwa mahojiano mtuhumiwa aliyetengeneza/andika maneno ya uvumi na
uzushi na kisha kuyasambaza katika mitandao ya kijamii kama FACEBOOK, WHATSAPP,
n.k kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Generali
DAVIS MWAMUNYANGE amenusurika kifo baada ya kulishwa sumu.
Baada ya taarifa hizo kupokelewa, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama kupitia dawati la makosa ya mitandao Makao
Makuu ya Polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walianza kufuatilia
mawasiliano ya kimtandao hadi ilipobainika nini chanzo cha taarifa hiyo. Baada
hapo msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa ulianza hadi tarehe 02/10/2015
alipokamatwa huko Arusha. Mtuhumiwa huyu jina lake linahifadhiwa kwa sababu za
kiupelelezi.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo ni mwanafunzi wa Mwaka
wa Kwanza katika moja ya Taasisis za elimu ya juu nchini. PiaBaada ya kukamatwa
alipekuliwa na kukutwa akiwa na Kompyuta Mpakato (LAPTOP) aina ya HP na simu ya
mkononi.
Aidha,katika mahojiano ya hayo mtuhumiwa amekiri kuusambaza ujumbe huo.
Upelelezi juu ya shauri hili unaendelea na utakapokamilika jalada la kesi hii
litafikishwa kwa mwanasheria wa serikali ili sheria ichukue mkondo wake.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment