Tume ya Taifa ya
uchaguzi nchini Tanzania imetakiwa kuhakikisha kuwa inaweka wazi mchakato mzima
wa upigaji kura na uesabuji wa kura hadi kupatikana kwa matokeo ili kuondoa
wasiwasi uliotanda kwa watanzania hususani vyama vya siasa kuhusu kuhofia zoezi
hilo kughubikwa na udanganyifu hali
inayoweza kusababisha vurugu wakati wa uchaguzi mkuu.
Kauli hiyo imekuja huku
kukiwa na wimbi la kauli mbalimbali za vyama kadhaa vya siasa kuhamasisha
wanachama na wapenzi wa vyama hivyo kupiga kura na kisha kulinda kura hizo kwa
kukaa meter mia moja kutoka katika vituo vya kupiga kura kwa kuhofia kuibiwa
kura zao kauli ambazo zimepingwa na tume ya taifa ya uchaguzi na kuwasihi
watanzania kuhakikisha kuwa hawafwati maagizo hayo kwani yanaweza
kuwasababishaia matatizo kutoka kwa vyombo vya dola.
-----------------
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dare s salaam kaimu mwenyekiti wa mtandao Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO wakati wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu IMELDA LULU URIO amesema kuwa ni kweli kuwa sheria ya uchaguzi inakataza watu kujikusanya karibu na maeneo ya vituo vya kupigia kura na wanatakiwa kuwa umbali wa meter mia moja sheria ambayo amesema bado haijaeleweka vizuri kwa watanzania walio wengi.
Amesema kuwa sheria inayoelekeza watu kukaa meter mia moja haikuwa na maana kuwa baada ya meter mia moja watu wakae na kulinda kura ila ina maana kuwa baada ya meter mia moja shughuli nyingine za kijamii zinaweza kuendelea huku akisema kinachotokea sasa ni kukosekana kwa elimu ya uraia kuhusu sheria hiyo inavyoelekeza.
Aidha amesema kuwa kauli ambazo zinatolewa na baadhi ya vyama vya siasa nchini Tanzania za kuwataka wafuasi wao kuhakikisha kuwa wanakaa katika hizo Meter mia moja na kulinda kura ni kiashiria kimoja wapo cha wazi kinachoonyesha kutokuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi ambapo ameitaka tume hiyo kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi changamoto hiyo na kuhakikisha kuwa wanaweka kila kitu wazi ili watanzania wawe na imani na tume hiyo kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania umekuwa ukifwatilia matukio mbalimbali yanayotokea katika harakati za kampeni za uchaguzi huo tangu kuzinduliwa kwake ambapo leo wametoa maswala kadhaa ambayo ni kasoro na vitendo vilivyo kinyume na kanuni za uchaguzi yanayojitokeza katika kampeni za uchaguzi huo.
Akizungumza na wanahabari leo Kaimu mwenyekiti wa TACCEO Bi IMELDA LULU URIO amesema kuwa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu mnamo tarehe 22 mwezi wa nane waangalizi wa mtandao huo wameweza kushughudia matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi na endepo kama hayatadhibitiwa mapema yanaweza kupelekea uvunjifu wa amani.
Akiyataja baadhi ya
matukio hayo amesema ni pamoja na matumizi ya lugha za dharau,matusi,na kejeli
zenye kuudhi baina ya wagombea wa vyama hasa vya CCM na muungano wa
UKAWA,matukio ya wafuasi kuvamia mikutano ya vyama vingine na kusababisha vurugu
na uvunjifu wa amani Mf tukio lililotokea huko mbeya la wafuasi wa chama cha
CHADEMA waliozuia msafara wa mgombea wa CCM mh MAGUFULI huku wakiimba na kuonyesha
ishara ya kutokumkubali,jambo ambali ameeleza kuwa matukio kama hayo yanaweza
kusababisha uvunjifu mkubwa wa amani.
Matukio mengine ambayo
TACCEO mpaka sasa wameyashughudia ni pamoja na Rushwa ambayo imeonekana kuwa ni
jambo la kawaida katika maeneo mengi kwa sasa,kampeni za usiku ambazo zimepewa
majina ya nyumba kwa nyumba,watoto /wanafunzi kutumika katika kampeni,matumizi
ya mali za uuma kwenye kampeni,uharibifu wa mabango ya wagombea,bendera,na mali
za vyama vya siasa,huku TACCEO wakisema yote hayo ni mambo ambayo yamejitokeza
sana katika muda huu wa kampeni na kama hayatafanyiwa kazi na wahusika yanaweza
kusababisha uvunjifu wa amani ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment