Mwenyekiti wa wabunge hao wa chama cha wananchi CUF ndugu JUMA HAMAD OMARY akizungumza |
Na Exaud Msaka Habari
Wabunge wa bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoka chama shiriki cha UKAWA chama cha
wananchi CUF wamesema kuwa hakuna mgogoro wa kisiasa unaoendelea zanzibar kama
inavyoelezwa na baadhi ya wanasiasa kwani uchaguzi wa Zanzibar umekamilika na
kinachosubiriwa ni kutangwaza kwa mshindi wa uchaguzi huo ili aweze kuanza kazi
mara moja.
Wabunge hao wamesema
kuwa hoja ya kuwahadaa watanzania kuwa visiwani huko kuna Mgogoro wa kisiasa ni
hoja iliyopandikizwa na chama cha mapinduzi ili waweze kuwaaminisha watanzania
kuwa kuna mgogoro jambo ambalo wamesema ni uzushi na kinachoendelea ni ulaghai
wa kutaka kupora ushindi alioupata mgombea wa chama hicho ndugu MAALIM SEIF
SHARIF HAMAD.
Mbunge wa jimbo la malindi Mh ALLY SALEHE akifafanua jambo |
Kaauli hiyo imetolewa
na wabunge hao Leo Jijini Dar es salaam katika makao makuu ya chama cha
wananchi CUF wakati wakitoa ufafanuzi wa kile kilichotokea Bungeni wakati Rais
wa Tanzania akifungua bunge ambapo
wabunge wa vyama vya upinzani wanaojulikana kwa jina La UKAWA waliamua kumpinga
wazi aliyekuwa Rais wa Zanzibar Dr shein na kuamua kutoka nje jambo ambalo
lilizua taharuki miongoni mwa wabunge ndani ya bunge hilo.
Mwenyekiti wa wabunge
hao wa chama cha wananchi CUF ndugu JUMA HAMAD OMARY amesema kuwa bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania lipo kwa mujibu wa sheria ambapo bunge hilo
linaendeshwa na sheria na kanuni zake na hivyo yanapotokea mambo ya kukiuka
kanuni na taratibu za bunge lazima wabunge hao watapaza sauti zao.
Amesema kuwa sheria
zinaeleza wazi kuwa anayeruhusiwa kuingia bungeni bila Ruhusa maalum ni Rais wa
Tanzania Pekee lakini wengine wanastahili kupata ruhusa ya wabunge wenyewe
ambapo amesema kuwa swala la Rais wa Zanzibar kuingia bungeni walishalipinga kw
barua kama utaratibu unavyoeleza lakini maombi yao yalizarauliwa na ndipo
walipoamua kumpinga wazi wazi mbela ya Dunia.
Amesema kuwa
wanachopinga na kupigania ni haki ya wanzanzibar inayotaka kuporwa na watu
wachache kwani wanaamini kuwa ili Rais Magufuli awe Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania ni lazima MAALIM SEIF SHARIF HAMAD atangazwe kuwa Rais wa Zanzibari
kwani kura zilizowachagua ni zile zile.
Amesema kuwa
kilichowafanya wabunge wa upinzani kupinga kuingia kwa viongozi wa zinzibar
bungeni Juzi ni kutetea katiba ya Zanzibar ambayo inasema muda wa Rais wa Zanzibar umekwisha malizika na
kukosa uhalali wa bunge kuedelea kukiwa hakuna uwakilishi iliokamilika kutoka
visiwani humo.
Akizungumza katika
mkutano huo na wanahabari mbunge wa jimbo la malindi Mh ALLY SALEHE amesema
kuwa katika vuta nikuvute ya Juzi bungeni spika wa bunge Mh JOB NDUGAI alivunja
kanuni za bunge kuwa kuruhusu askari wa kawaida zaidi ya 40 ikiwa ni pamoja na
mlinzi wa Rais aliyetumika kuleta bahasha yenye jina la waziri mkuu kuingia
ndani ya bunge kinyume na sheria jambo ambali amesema lilihitaji maombi maalumu
na yaridhiwe na bunge nzima ndipo afanye hivyo.
Wabunge hao wameapa
kuhakikisha kuwa wanapigania haki ya wanzanziabari juu ya Rais waliyemchagua
ndani na nje ya bunge hadi kuhakikisha kuwa Mgombea wa chama Cha wananchi Cuf
anatangazwa kuwa Rais wa zanzibar
No comments:
Post a Comment