Monday, December 7, 2015

Breaking News-Rais Magufuli atimua wengine muda huu Bandarini na katibu mkuu uchukuzi--soma hii

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa taarifa kuwa Rais John Magufuli amevunja bodi ya Bandari na ametengua nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi Profesa Joseph Msamichaka. Amefukuzs kazi watendaji wote waliohusika na kupokea na kutoa makontena kwenye bandari kavu ICD' pia amemsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka baada ya kushindwa kusimamia fedha za TRL kiasi cha Sh Bil 16.KATIKA kile kinachoonekana kutotaka masikhara na uzembe uzembe katika Serikali yake,Rais Dr John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Bandari Awadh Massawe pamoja na Mwenyekiti wa bodi Mhandisi Prof. Joseph Msambichaka 
Taarifa zinasema kuwa Dr Magufuli ameamua kufanya hivyo kutokana na uzembe uliokithiri wa baadhi ya maofisa wa bandari ambao umechangia Serikali kupoteza mabilioni ya fedha kwa kutowadai kodi wafanyabaishara waliokuwa wakiitumia bandari kama kichaka chao
Aidha mwingine aliyekubwa na dhoruba hiyo ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka

No comments: